Pata taarifa kuu
UFILIPINO-SIASA

Ufilipino: Rais Duterte atangaza kustaafu siasa

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amesema hatowania tena urais wakati wa Uchaguzi Mkuu  mwaka ujao na atastaafu siasa baada ya muhula wake kuisha.

Rais wa Ufilipino  Rodrigo Duterte
Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte Noel CELIS AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Duterte ametoa tangazo hilo la kushangaza akiwa na mshirika wake wa karibu na wa siku nyingi Seneta, Bong Go, alikwenda kuwasilisha fomu za kuwania umakamu wa rais kwa Tume ya Uchaguzi.

Kiongozi huyo ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2016, amesema anatangaza kustaafu siasa na hawezi kuwania tena uongozi wa nchi hiyo kwa sababu itakuwa ni kinyume cha Katiba ya nchi hiyo.

Nchini Ufiulipino, rais anaongoza nchi hiyo kwa muhula mmoja wa miaka sita, lakini kabla ya tangazo la rais Duterte kulikuwa na taarifa kuwa alikuwa anataka kuwania nafasi ya Makamu wa rais lakini pia alikuwa anaweka mikakati ya kutaka binti yake amrithi.

Wale wanaotaka kuwania urais, wana mpaka Ijumaa wiki ijayo kuwasilisha majina yao kwenye Tume ya Uchaguzi, wakati huu mwanamasumbwi Manny Pacquiao ambaye wiki hii alistaafu kwenye mchezo huo, tayari amewasilisha ombo la kuwania urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.