Pata taarifa kuu

Ressa na Muratov kushinda Tuzo ya amani ya Nobel uhuru wa kujieleza

Waandishi wa Habari Maria Ressa kutoka nchini Ufilipino na Dmitry Muratov, kutoka Urusi ndio washindi wa mwaka huu wa Tuzo ya amani ya Nobel, kutokana na juhudi zao za kulinda uhuru wa kujieleza katika mazingira magumu.

Tuzo ya Amani ya Amani ya 2021 imetolewa kwa waandishi wa habari Maria Ressa na Dimitri Muratov.
Tuzo ya Amani ya Amani ya 2021 imetolewa kwa waandishi wa habari Maria Ressa na Dimitri Muratov. © REUTERS/Eloisa Lopez/ REUTERS/Sergei Karpukhin
Matangazo ya kibiashara

Kamati inayotoa tuzo hiyo ya amani ya Nobel, imesema wawili hao wametambuliwa na kuibuka washindi kufuatia, kazi kubwa ambayo wamekuwa wakifanya nchini Ufilipino na Urusi, kupigania haki ya kujieleza.

Ressa, mwandishi wa zamani wa CNN ambaye pia ana uraia wa Marekani, ameendelea kufanya kazi kwenye mazingira magumu na wakati wa tuzo hii, amekataa rufaa Mahakamani kupinga, inayomkabili dhidi ya serikali ya Ufilipino.

Naye, Muratov, mwenye umri wa miaka 59,,amekuwa akitetea haki ya kujieleza na wanahabari kufanya kazi zao nchini Urusi licha ya mazingira mazgumu.

Mwaka 1993, alianzisha Gazeti alilolipa jina Novaya Gazeta, ambalo limekuwa katika mstari wa mbele kuikosoa serikali, hatua ambayo imepelekea wanahabari wa Gazeti hilo kuuawa, kutishwa na hata kushambuliwa.

Hata hivyo, Urusi imempongeza Muratov, licha ya Gazeti lake kuwa katika mstari wa mbele kuipinga serikali nchini humo.

Mwaka uliopita, tuzo hii ilichukuliwa na Shirika la Mpango wa Chakula duniani WFP kutokana na juhudi zake za kusaidia kupambana na baa la njaa duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.