Pata taarifa kuu

Idadi ya vifo yaongezeka baada ya kimbunga kikali cha Rai kupiga Ufilipino

Takriban watu 33 wameuawa na kimbunga chenye nguvu zaidi kuwahi kuikumba Ufilipino mwaka huu, na wengine kadhaa hawajulikani walipo, mamlaka imesema Jumamosi hii. mamlaka nchini Ufilipino imeripoti uharibifu "wa kutisha" nchini humo.

Kimbunga Rai kimefanya uharibifu mkubwa Ufilipino.
Kimbunga Rai kimefanya uharibifu mkubwa Ufilipino. AP - Jay Labra
Matangazo ya kibiashara

Rai ilielezewa kama "kimbunga kikubwa" kilipotua Alhamisi, kwenye kisiwa cha kitalii cha Siargao, kikiambatana na upepo wa 195 km kwa saa. "Kila kitu kilikuwa kikipa hewani, ilikuwa kana kwamba ulikuwa mwisho wa dunia," alishuhudia Raphy Repdos, mwendeshaji wa watalii aliyetembelea kisiwa hicho wakati wa dhoruba.

Zaidi ya watu 300,000 wamelazimika kutoroka makazi yao tangu Alhamisi wiki hii kwa sababu ya kimbunga kilichoharibu kusini na katikati mwa nchi, kulingana na Shirika la Majanga ya Asili nchini  Ufilipino.

Picha za angani zilizoruswa na wanajeshi zimeonyesha uharibifu mkubwa katika mji wa Jenerali Luna, ambapo wasafiri na watalii wengi walikuwa wamemiminika kabla ya Krismasi, huku majengo yasiyo na paa na vifusi vikiwa vimedondoka chini.

"Kuta na paa zimeng'olewa na kupeperushwa kama karatasi"

Kisiwa jirani cha Dinagat "kiliathirika" na dhoruba hiyo, Gavana Arlene Bag-ao aliandika amesema kwenye ukurasa wake wa Facebook, akiongeza kuwa nyumba, boti na mashamba vimeharibiwa. "Kuta na paa ziling'olewa na Odette kama karatasi," alisema, akitumia jina hilo la kimbunga Rai linalotumiwa na wakaazi wa mkoa huo.

Alberto Bocanegra, mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mashirika ya Msalaba Mwekundu na Hilali nyekundu amesema: “Hii ni mojawapo ya dhoruba zenye nguvu zaidi kuwahi kuikumba Ufilipino mwezi wa Desemba katika mwongo mmoja uliopita, ” huku akiongeza "taarifa tunazopokea na picha tunazopokea ni za kutisha sana."

Zaidi ya wanajeshi 18,000, maafisa polisi, walinzi wa pwani na maafisa wa Wazima Moto watajiunga katika juhudi za utafutaji na uokoaji katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi, ametangaza Mark Timbal, msemaji wa idara ya majanga nchini Ufilipino.

Idadi hiyo iliongezeka baada ya tangazo la mkuu wa majanga ya asili wa jimbo la kati la Negros Occidental, ambaye amethibitisha vifo vya watu 13, wengi wao kwa kuzama, na kutoweka kwa wengine 50 katika eneo lililoathiriwa na mafuriko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.