Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-HAKI

Australia: Mahakama yakataa rufaa ya Bingwa wa Tennis duniani kupinga kufukuzwa kwake

Mahakama ya Shirikisho la Australia siku ya Jumapili Januari 16 ilikataa rufaa iliyoletwa na Bingwa wa Tennis duniani Novak Djokovic dhidi ya kufutwa kwa visa yake na kufukuzwa nchini.

Novak Djokovic anafanya mazoezi kwa kujiandalia michuano ya Tennis ya Australian Open, ambayo hataweza kushiriki, Januari 14, 2022.
Novak Djokovic anafanya mazoezi kwa kujiandalia michuano ya Tennis ya Australian Open, ambayo hataweza kushiriki, Januari 14, 2022. MARTIN KEEP AFP
Matangazo ya kibiashara

"Mahakama inaamuru kwamba rufaa itupiliwe mbali kwa gharama ya mlalamikaji," umebaini uamuzi huo ulioidhinishwa kwa kauli moja na majaji watatu, katika mkesha wa kuanza kwa michuano ya Tennis ya Australian Open. Mserbia huyo alikuwa amenuia kutafuta taji la 21 la Grand Slam katika michuano hiyo inayopigwa nchini Australian.

Majaji watatu wa Mahakama hiyo walisikiliza kwa saa nne hoja za wawakilishi wa Bingwa huyo wa Tennis duniani na zile za serikali, kabla ya kuondoka katika chumba cha mahakama kwa minajili ya kuchukuwa uamuzi.

Katika hitimisho lake alilowasilisha Jumamosi mbele ya Mahakama, Waziri wa Uhamiaji Alex Hawke alibaini kwamba kuwepo kwa Djokovic nchini "kuna uwezekano wa kusababisha hatari ya afya". Amesema kumkubalia Novak Djokovic kubaki nchini humo na kushiriki michuano hii itaongeza"hisia za kupinga chanjo" na inaweza kuwazuia Waaustralia kupata chanjo zao za nyongeza wakati kirusi kipya cha Omicron kinaendelea kusambaa kwa kasi nchini kote.

Mfano mbaya kwa serikali ya Australia

Uwepo nchini Australia wa Novak Djokovic unaweza hata "kusababisha kuongezeka kwa machafuko ya wenyewe kwa wenyewe", alibaini waziri. Waziri aliongeza kwamba "dharau" yake kwa hatua za afya dhidi ya Covid ni mfano mbaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.