Bingwa wa mchezo wa Tennis duniani Novak Djokovic azuiwa kuingia Australia
Serikali ya Australia imefuta kibali cha kuingia nchini humo cha bingwa wa mchezo wa Tennis duniani Mserbia Novak Djokovic, kufuatilia kile ambacho maafisa nchini humo wanasema mchezaji huyo hakutimiza masharti ya kuingia nchini humo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Hii imekuja baada ya mchezaji huyo kusema amepata msamaha wa kuingia nchini Australia kushiriki kwenye michezo ya Australia Open kuanzia Januari 17 bila ya kuwa na cheti cha kuonesha kuwa amepata chanjo.
Waziri Mkuu Scott Morrison amesema sheria lazima ziheshimiwe.
Djokovic hata hivyo hajazungumzia lolote kuhusu iwapo amechanjwa, ila mwaka uliopita, alisema alikuwa haungi mkono chanjo.