Pata taarifa kuu
CHINA-ASILI

China yaahidi kutoa euro milioni 200 kwa ajili ya mradi wa bioanuwai

Majadiliano yanaendelea Jumanne huko Kunming, nchini China, ambayo ni mwenyeji wa mkutano wa 15 wa kuhusu vita dhidi ya kutoweka kwa spishi.

Rais wa China Xi amteangaza kwamba China imeahidi kutoa euro Milioni 200 kwa ajili ya mradi wa bioanuwai kwenye mataifa yanayoendelea.
Rais wa China Xi amteangaza kwamba China imeahidi kutoa euro Milioni 200 kwa ajili ya mradi wa bioanuwai kwenye mataifa yanayoendelea. AFP - STR
Matangazo ya kibiashara

Rais wa China Xi Jinping ametangaza kuzindua mfuko uliopewa na Beijing kwa euro milioni 200 kusaidia ulinzi wa bioanuai katika nchi zinazoendelea.

Katika ufunguzi wa mkutano huo, COP15, China imetangaza Jumanne, Oktoba 12, kuundwa kwa mfuko mpya wa euro milioni 200 kulinda bioanuwai katika nchi zinazoendelea.

"China itachukua hatua ya kuanzisha Mfuko wa Viumbe anuwai wa Kunming kwa mchango wa yuan bilioni 1.5 (sawa na euro milioni 200) kusaidia uhifadhi wa bioanuai katika nchi zinazoendelea," rais wa China Xi Jinping amesema katika mkutano huo huko Kunming, kusini magharibi mwa China. "China inatoa wito kwa (...) pande zote kuchangia mfuko huo," ameongeza.

Tangazo lililotolewa na China "ni hatua ya kwanza kukaribishwa", amesema Georgina Chandler, kutoka shirika lisilo la kiserikali la Royal Society for protection of birds, lakini jumla ya euro milioni 200 "haitoshi kuziba pengo." Pengo la kifedha linalohitajika kwa bioanuai ".

Mfumo mpya wa kulinda asili kuanza kabla ya 2030

Kwa sababu ya janga la Covid-19, COP15 imefanyika mkondoni mwaka huu, na hatua zilizorekodiwa hapo awali na marais wa Urusi Vladimir Poutine, wa Ufaransa Emmanuel Macron, wa Costa RicaC arlos Alvarado na wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ambaye nchi yake itakuwa mwenyeji wa mkutano kuhusu bioanuwai, COP16.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.