Pata taarifa kuu
TAIWAN-USALAMA

Taipei: Ndege 38 zaingia katika eneo letu la ulinzi

Idadi kubwa ya ndege za jeshi la China ziliingia kwenye anga ya ulinzi ya Taiwan Ijumaa, Oktoba 1. Luteka hii ya kijeshi ni sehemu ya muktadha wa kuongezeka kwa vitisho vya Beijing dhidi ya Taiwan, kisiwa cheny wakaazi Milioni 4, kilio chini ya mifumo yakidemokrasia ambacho kinajitawala. China imekiri kufanya lutekahiyo nakuingiza ndege zake kwenye anga ya Taiwan.

Ndege ya kivita ya China J-16, iliyopigwa picha na jeshi la Taiwan.
Ndege ya kivita ya China J-16, iliyopigwa picha na jeshi la Taiwan. AP
Matangazo ya kibiashara

Ndege 38, pamoja na ndege mbili zenye uwezo wa kubeba silaha za nyuklia. Hii ndio idadi ya ndege za jeshi la China zilizotambuliwa Ijumaa hii na jeshi la Taiwan katika anga yake ya ulinzi.

Hiki ni kitendo cha "uchokozi" iikiwa kama sehemu ya mkakati wa "unyanyasaji" wa Beijing, Waziri Mkuu wa Taiwan amesema Jumamosi hii asubuhi.

Luteka hii ya China imekuwa ikifanyika karibu kila siku tangu kuchaguliwa tena kwa rais Tsai Ing-wen mwezi Januari 2020. Kama wakaazi wengi wa Taiwan, kiongozi huyo anafutilia mbali madai ya China kuwa kisiwa hicho ni sehemu ya ardhi ya Beijing.

China inaiona Taiwan yenye demokrasia kama jimbo lililojitenga, lakini Taiwan inajiona kama taifa huru.

Taiwan imekuwa ikilalamika kwa zaidi ya mwaka mmoja juu ya harakati za kijeshi za mara kwa mara za vikosi vya anga vya China karibu na kisiwa hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.