Pata taarifa kuu
UFARANSA-USHIRIKIANO

Ununuzi wa manowari: Mawaziri wa EU washikamana na Paris dhidi ya Washington

Nchi za Umoja wa Ulaya "zimeonyesha uungwaji wao mkono na msikamano " kwa Ufaransa katika mzozo wa manowari kati yake na Marekani, Mkuu wa seza za Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya Joseph Borrell.

Mkuu wa seza za Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya Joseph Borrell.
Mkuu wa seza za Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya Joseph Borrell. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wa Mambo ya nje wa kutoka nchi ishirini na saba wanachama wa Umoja w Ulaya, waliokutana mjini New York, nchini Marekani, kando ya Mkutano Mkuu wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa, "walielezea wazi mshikamano wao na Ufaransa", "uungwaji mkono ulio dhahiri", Josep Borrell aliwaambia waandishi wa habari.

Mgogoro unaohusiana na kuvunjika kwa makubaliano kabambe ya ununuzi wa manowari za Ufaransa kwa euro bilioni 56 unaendelea kutotoka. Ufaransa inailaumu Australia kuvunja mkataba huo kwa maksudi na kufanya ushirikiano mpya wa usalama na Marekani na Uingereza.

Wiki iliyopita, Marekani ilitangaza kuhusu makubaliano ya usalama ya nchi tatu, kama sehemu ya ushirikiano wa kimkamati ambapo nyambizi za nyuklia za Marekani zitapelekwa nchini Australia.

Nchi tatu za muungano uliopewa jina la AUKUS sasa zinajaribu kuihakikishia Paris. Hivi karibuni rais wa Marekani alitoa wito wa kumtaka rais wa Ufaransa, na Uingereza na Australia kujaribu kutuliza hali hii ambayo haioneshi sura nzuri kwa dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.