Pata taarifa kuu
UFARANSA-USHIRIKIANO

Taharuki yatanda kati ya Ufaransa na nchi za muungano wa AUKUS

Mgogoro unaohusiana na kuvunjika kwa makubaliano kabambe ya ununuzi wa manowari za Ufaransa kwa euro bilioni 56 unaendelea kutotoka. Ufaransa inailaumu Australia kuvunja mkataba huo kwa maksudi na kufanya ushirikianom pya wa usalama na Marekani na Uingereza.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Malcolm Turnbull (wakati huo Waziri Mkuu wa Australia) huko Sydney Mei 2018 (picha ya kumbukumbu). Uhusiano ulikuwa mzuri kati ya Paris na Canberra wakati huo.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Malcolm Turnbull (wakati huo Waziri Mkuu wa Australia) huko Sydney Mei 2018 (picha ya kumbukumbu). Uhusiano ulikuwa mzuri kati ya Paris na Canberra wakati huo. BRENDAN ESPOSITO POOL/AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa Canberra wa kufuta mkataba huu kwa niaba ya manowari za Marekani umighadhabisha Ufaransa.

Wiki iliyopita, Marekani ilitangaza kuhusu makubaliano ya usalama ya nchi tatu, kama sehemu ya ushirikiano wa kimkamati ambapo nyambizi za nyuklia za Marekani zitapelekwa nchini Australia.

Nchi tatu za muungano uliopewa jina la AUKUS sasa zinajaribu kuihakikishia Paris. Rais wa Marekani ametoa wito wa kumtaka rais wa Ufaransa, na Uingereza na Australia kujaribu kutuliza hali hii ambayo haioneshi sura nzuri kwa dunia.

Kwa upande mmoja, Waziri Mkuu wa Uingereza amesisitiza umuhimu mkubwa wa uhusiano wake na jirani yake Ufaransa, akiibua upendo wa London "usioweza kuepukika" kwa Paris. Boris Johnson amejaribu kuihakikishia Ufaransa kwa kuelezea kuwa AUKUS - ushirikiano wa kimkakati uliotiwa saini wiki iliyopita kukabiliana na China - haungeweza "kuepukika" na kwamba Paris haifai "kuwa na wasiwasi".

Australia, kwa upande wake, imetangaza Jumatatu hii, Septemba 20, kwamba makumi ya maelfu ya Waaustralia waliuawa kwenye ardhi ya Ufaransa kwa kulinda nchi hiyo  wakati wa Vita vya Kwanza na vya Pili vya Dunia, na hivyo kuelezea mshikamano wake na Ufaransa, kulingana na serikali ya Australia.

Korea Kaskazini yapinga mkataba mpya kati ya Marekani, Uingereza na Australia

Wakati huo huo Korea Kaskazini kupitia wizara yake ya Mambo ya Nje, imesema leo kuwa ushirikiano wa kijeshi wa Marekani, Australia na Uingereza unaohusisha nyambizi, kwenye ukanda wa Indo-Pasifiki unaweza kusababisha ushindani wa silaha za nyuklia kwenye ukanda huo, na kuongeza kwamba hatua hiyo inaonesha kwamba Marekani ndiyo mhalifu mkuu wa mfumo wa kimataifa wa kuzuia matumizi ya silaha za nyuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.