Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-ULINZI

Canberra: Tuko wakweli na waaminifu na tunafanya mambo yetu kwa uwazi

Katika kesi ya manowari kati ya Ufaransa na Australia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean Yves le Drian, ameshtumu Australia kwa uwongo Jumamosi jioni Septemba 18 na kubaini kwamba sasa kuna mgogoro na nchi hii, lakini pia Marekani.

Waziri wa Ulinzi wa Australia Peter Dutton (picha yetu), katika mahojiano na Sky News, alipinga shutuma za Ufaransa za usaliti: "Tuko wakweli, waaminifuna tulifanya mambo yetu kwa uwazi".
Waziri wa Ulinzi wa Australia Peter Dutton (picha yetu), katika mahojiano na Sky News, alipinga shutuma za Ufaransa za usaliti: "Tuko wakweli, waaminifuna tulifanya mambo yetu kwa uwazi". MANDEL NGAN AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Waziri wa Ulinzi wa Australia, Peter Dutton, ambaye yuko ziarani nchini Marekani, kwa upande wake, amehakikisha kwamba serikali yake iko sawa na wala haiwezi kulaumiwa na Ufaransa.

Serikali ya Australia, kupitia sauti ya Waziri wake wa Ulinzi, Peter Dutton, ambaye katika mahojiano na Sky News amepinga shutma za Ufaransa kwamba Australia imefanya uhaini: "Tuko wakweli, waaminifu na tulifanya mambo yetu kwa uwazi. Wasiwasi wetu uko hadharani, kila mtu anaweza kuchunguza hilo. Hata hivyo, Ufaransa ilikuwa na wasiwasi sana kwamba ilituma jemadari kukutana nasi wiki mbili zilizopita. "

Teknolojia ya Ufaransa haikukidhi mahitaji ya Australia

Waziri wa Ulinzi wa Australia ameongeza pia kwamba hata kama Ufaransa ingekuwa tayari kuchangia teknolojia yake ya nyuklia na Australia, isingeweza kukidhi mahitaji ya Australia. "Hatuna tasnia ya nyuklia katika nchi yetu," amesema Dutton. Walakini, mtindo wa Ufaransa, mtindo wa Barracuda, unatakiwa kurekebishwa kila baada ya miaka 7 hadi 10. Wakati teknolojia inayotumiwa na Uingereza na Marekani, mtambo huo unaendelea kufanya kazi kwa miaka 35. "

Scott Morrison atasafiri pamoja na wenzake wa India na Japan, kwenda Washington wiki ijayo kwa mkutano wa Quad, muungano huo katika ukanda wa Indo Pacific ambao Ufaransa sio mwanachama.

Katika Asia ya Kusini-Mashariki, hata hivyo, mkataba wa ushirikiano wa kiusalama kati ya Australia, Marekani na Uingereza unatia wasiwasi nchi jirani, amesema mwandishi wetu katika eneo hilo, Gabrielle Maréchaux. Katika eneo hili lililojikuta kati ya ushawishi wa Marekani na nchi jirani ya China, Malaysia na Indonesia wameelezea wasiwasi wao kuhusu mbio hizi mpya kuhusiana na silaha.

Neno "nyuklia" latisha

Wakati wa mazungumzo na mwenzake wa Australia, Waziri Mkuu wa Malaysia alielezea hofu yake kwamba muungano huu mpya kati ya Australia na Marekani utashawishi nchi zingine zenye nguvu kuchukua hatua kali zaidi katika eneo hilo, akimaanisha Beijing. Ikiwa neno "nyuklia" linatisha sana leo, pia linapingana na msimamo wa Asean, ambayo tangu Mkataba wa Bangkok wa 1995 ilijikubalisha kufanya ukanda huo kuwa eneo lisilo na silaha za nyuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.