Pata taarifa kuu
UFARANSA-USHIRIKIANO

Paris yawarejesha nyumbani mabalozi wake wa Washington na Canberra

Baada ya kutangazwa kwa ushirikiano wa kimkakati kati ya Washington, London na Canberra, na kusababisha kufutwa kwa Australia kwa mkataba wa ununuzi wa manowari kutoka Ufaransa, Paris imetangaza kuwarejesha nyumbani mabalozi wake wa Marekani na Australia kwa mashauriano.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian (hapa ilikuwa Septemba 10 nchini Ujerumani) ametetea uamuzi wa Ufaransa wa kuwarejesha mabalozi wake Marekani na Australia kufuatia uzito wa maneno yaliyotolewa na Washington na Canberra.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian (hapa ilikuwa Septemba 10 nchini Ujerumani) ametetea uamuzi wa Ufaransa wa kuwarejesha mabalozi wake Marekani na Australia kufuatia uzito wa maneno yaliyotolewa na Washington na Canberra. AP - Jens Schlueter
Matangazo ya kibiashara

Kihistoria, kwa mara ya kwanza, Ufaransa inawarejesha nyumbani mabalozi wake wa Washington na Canberra. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian ametetea uamuzi huu "wa kipekee", uliofanywa kwa ombi la rais Emmanuel Macron, "kufuatia kauli za kibri zilizotolewa na Australia na Marekani Septemba 15".

Rais atakutana na mabalozi wawili ambao wanarudi Ufaransa kutathmini hali pamoja nao. Ikiwa mgogoro na Marekani na Australia umekuwa wasiwasi mkubwa kwa rais wa Ufaransa tangu Jumatano, hakutaja hadharani jambo hili wakati wa ziara yake huko Athenes kwa mkutano wa EU-MED, ameripoti mwandishi wetu maalum huko Athenes, Valérie Gesi.

Sababu kuu ni tangazo lililotolewa Jumatano na Joe Biden la ushirikiano wa usalama na Australia na Uingereza. Ushirikiano huu, ambao ni pamoja na kuipa Australia manowari zinazotumiwa kwa nyuklia, jambo hilo lisababisha kufutwa kwa Canberra kwa mkataba mkubwa uliyosainiwa na Paris mnamo 2016 kwa kuizuia Astralia manowari kumi na mbili kutoka Ufaransa.

Siku ya Alhamisi, Jean-Yves Le Drian alishutumu Australia na uamuzi "wa ghafla" wa rais wa Marekani Joe Biden ambaye, kulingana na Paris, hakutaka kushauriana na Ufaransa kabla ya tangazo lake.

Kwenye RFI, Waziri wa Vikosi vya Wanajeshi Florence Parly alikosoa kile alichokiita "taarifa mbaya sana kwa heshima ya kauli iliyotolewa" na uamuzi "mzito" kulingana na sera ya kimataifa.

Hisia ya usaliti kwa upande wa Ufaransa ni muhimu sana na uamuzi huu wa kuwarejesha nyumbani mabalozi wake unakusudia kuifanya Marekani na Australia kuelewa kuwa Ufaransa imeghadhabishwa na kitendo walichokifanya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.