Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-USHIRIKIANO

Ufaransa na Australia zaimarisha ushirikiano wao wa kijeshi Indo-Pacific

Ufaransa na Australia hivi sasa zinakamilisha mazungumzo ya kuimarishwa kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili, kwa lengo la kuhakikisha usalama katika eneo la Indo-Pacific, ambapo shinikizo kutoka China inaendelea kutia wasiwasi nchi hizo.

Wanajeshi wa Australia wakati wa mafunzo ya pamoja na Marekani huko Queensland Julai 2019.
Wanajeshi wa Australia wakati wa mafunzo ya pamoja na Marekani huko Queensland Julai 2019. REUTERS - JASON REED
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi wa Ufaransa na meli za kivita zimewekwa katika kambi za jeshi la Australia.Nchi hizo mbili kwa sasa zinajadili masharti ya makubaliano ya kijeshi ambayo yanaweza kupelekea Ufaransa kuwa mshirika wa karibu zaidi wa Australia baada ya Marekani.

Ushirikiano huu unakuja wakati China ambae ni mshirika mkuu wa biashara wa Australia imekuwa ikitoa shiniko kwa nchi hiyo. Kulingana na Peter Jennings, mkurugenzi wa Taasisi ya Sera ya Mkakati ya Australia, anasema hii ndio sababu Canberra imeamua kuimarisha ushirikiano na Ufaransa. "Nadhani moja ya sababu ya shinikizo kutoka kwa China imepelekea kukuza uhusiano wa karibu na nchi kuu za Ulaya," amebbaini.

Ufaransa, ambayo ina ushirikiano na majimbo ya New Caledonia na French Polynesia, inaonekana kama mshirika mkubwa nchini Australia, ambayo imeinunulia manowari kumi na mbili.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa upande wake, hivi karibuni alibaini kwamba anataka kukuza ushirikiano wa Ufaransa katika sehemu hii ya dunia. Kwa kweli, wanajeshi kutoka Ufaransa kwa sasa wanafanya mazoezi huko Queensland na wenzao wa Australia. Kikosi cha Anga kitashiriki mazoezi ya pamoja ya kijeshi mwaka ujao na Jeshi la Wanamaji litafanya vivyo hivyo mnamo mwaka 2023, pamoja na Australia lakini pia na Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.