Pata taarifa kuu
TAIWAN-USALAMA

Taiwan yakaribisha muungano kati ya Canberra, Washington na London

Marekani na Australia zimeahidi "kuimarisha uhusiano" na Taiwan, ambayo inatishiwa na uvamizi wa Beijing. Serikali ya Taiwan, kwa upande wake, "imekaribisha" makubaliano mapya kati ya nchi hizo tatu, ambayo "inachangia masilahi sawa ya amani na utulivu".

Mazoezi ya jeshi la Taiwan kukabili uvamizi wa China, Septemba 16, 2021.
Mazoezi ya jeshi la Taiwan kukabili uvamizi wa China, Septemba 16, 2021. AP
Matangazo ya kibiashara

Maneno ya serikali ya Taiwan ni ya tahadhari, lakini mkataba mpya kati ya nchi hio tatu unaweza tu kuwa habari njema kwa Taipei. Chini ya kilomita 200 kutoka pwani ya China, Taiwan inakabiliwa na shinikizo kubwa katika miaka ya hivi karibuni kutoka Beijing, ambayo haifichi nia yake ya kuidhibiti Taiwan kama moja ya sehemu yake ya ardhi.

Siku ya Ijumaa, ndege kumi za jeshi la China zilipita juu ya anga la Taiwan, kwani jeshi la Taiwan limekamilisha mazoezi ya kijeshi ya siku tano yaliyopangwa kukabiliana na uvamizi wa China.

Kwa kuweka utulivu katika ukanda wa Indo-Pacific katikati ya muungano huu mpya, makubaliano kati ya serikali hizo tatu yanaleta dhamana mpya ya usalama kwa Taiwan.

"Taiwan imekuwa ikishirikiana kwa muda mrefu kwa amani na utulivu katika eneo la Indo-Pacific na Marekani, Australia na Uingereza," amesema Joanne Ou, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Taiwan. Tutaendelea kuimarisha uhusiano wetu na Washington na nchi zingine washirika ili kulinda amani kwa pamoja katika Mlango wa Taiwan. "

Taiwan imetajwa mara nne katika taarifa ya pamoja kati ya Washington na Canberra. Mamlaka hizo mbili zinasisitiza juu ya nia yao ya "kuimarisha uhusiano wao na Taiwan".

Baada ya ule wa Japani, msaada huu ni onyo kubwa kwa China. Hasa kwa kuwa inakuja juu ya habari nyingine nzuri kwa Taiwan, wakati huu ikitoka Umoja wa Ulaya, ambao wiki hii ulitangaza mkakati wake katika ukanda wa Indo-Pacific, ambao pia unalenga skukatisha matamanio ya China.

Bunge la Ulaya lilipitisha azimio Alhamisi (Septemba 16) kuonya sera ya "upanuzi" wa China katika ukanda wa Pasifiki na kutetea makubaliano ya uwekezaji na Taiwan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.