Pata taarifa kuu
CHINA-USALAMA

China yakosoa muungano mpya wa kijeshi kati ya Marekani ,Uingereza na Australia

China imelaani ushirika mpya wa usalama wa kihistoria kati ya Marekani, Uingereza na Australia. China imeutaja muungano huo kuwa wenye maono yasiofaa'.

Viongozi wa Marekani, Uingereza na Australia wameutangaza ushirika huo mpya ili kuzuia kile kinachotafsiriwa kama hatua ya kukabiliana na ushawishi wa China unaozidi kupanuka katika ukanda wa Indo-Pasifiki.
Viongozi wa Marekani, Uingereza na Australia wameutangaza ushirika huo mpya ili kuzuia kile kinachotafsiriwa kama hatua ya kukabiliana na ushawishi wa China unaozidi kupanuka katika ukanda wa Indo-Pasifiki. AP
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano hayo yatazifanya Marekani na Uingereza kuipatia Australia teknolojia ya kujenga manowari zenye uwezo wa kinyuklia kwa mara ya kwanza.

Kundwa kwa muungano huu inaonekana kama juhudi za kuukabili ushawishi wa China katika eneo la kusini mwa China linalozozaniwa.

Wakati huo huo Umoja wa Ulaya umesema haukuarifishwa kuhusu kuundwa kwa ushirika mpya wa kijeshi kati ya Marekani, Uingereza na Australia, kwa mujibu wa msemaji wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Peter Stano, huku akiongeza kwamba watajaribu kuzungumza na Marekani, Uingereza na Australia ili kujua kinachoendelea.

Peter Stano amebaini kwamba nchi za Ulaya zitajadiliana kuhusu athari ya uamuzi wa nchi hizo tatu.

Viongozi wa Marekani, Uingereza na Australia wameutangaza ushirika huo mpya ili kuzuia kile kinachotafsiriwa kama hatua ya kukabiliana na ushawishi wa China unaozidi kupanuka katika ukanda wa Indo-Pasifiki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.