Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI

Marekani yaondoa vikwazo vinavyohusiana na mradi wa Nord Stream 2

Utawala wa Rais wa Mrekani Joe Biden ulikuwa umeweka vikwazo kwa kampuni inayohusika na mradi wa bomba la mafuta la Nord Stream 2 na kwa vingozi wa kampuni hii, lakini mara moja imeondoa vikwazo hivyo kwa sababu ya wasiwasi wa usalama wa kitaifa, imebaini ripoti ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani.

Joe Biden anapinga mradi wa bomba la mafuta la Nord Stream 2, uliofadhiliwa na kampuni kubwa ya gesi inayomilikiwa na serikali ya Urusi, Gazprom, na ambapo kazi yake imekamilika karibu 95% kwa, akiiona kama ni mpango mbaya kwa Ulaya.
Joe Biden anapinga mradi wa bomba la mafuta la Nord Stream 2, uliofadhiliwa na kampuni kubwa ya gesi inayomilikiwa na serikali ya Urusi, Gazprom, na ambapo kazi yake imekamilika karibu 95% kwa, akiiona kama ni mpango mbaya kwa Ulaya. Odd ANDERSEN AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Hati hiyo, iliyopelekwa kwa Bunge la Marekani na ambayo shirikala habari la Reuters limepata kopi, inabaini kwamba kampuni inayosimamia mradi unaotarajia kuunganisha Urusi na Ujerumani na mkurugenzi wake mkuu, Matthias Warnig, ambaye ni mshirika wa karibu wa Rais wa Urusi Vladimir Putin, ambaye alikuwa anakabiliwana vikwazo hivyo, Marekani imeamua kuviondoa kwa masilahi ya taifa.

Hatua hiyo inakuja wakati utawala wa Joe Biden kutoka chama cha Democratic, madarakani, tangu mwezi Januari mwaka huu, unajaribu kuanzisha tena uhusiano na Ujerumani uliyoharibiwa na rais wa zamani Donald Trump kutoka chama cha Republican.

Joe Biden anapinga mradi wa bomba la mafuta la Nord Stream 2, uliofadhiliwa na kampuni kubwa ya gesi inayomilikiwa na serikali ya Urusi, Gazprom, na ambapo kazi yake imekamilika karibu 95% kwa, akiiona kama ni mpango mbaya kwa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.