Pata taarifa kuu
URUSI

Mvutano waibuka kati ya Urusi na Marekani juu ya Bahari ya Pasifiki

Urusi na Marekani kwa kila upande wametuma ndege za kivita kusindikiza ndege kutoka upande mwingine juu ya Bahari ya Pasifiki, mashirika ya habari ya Urusi yameripoti Ijumaa.

Ndege ya upelelezi ya kikosi cha anga cha  Marekani RC-135 ikiruka juu ya Bahari ya Pasifiki karibu na pwani ya Kamchatka Aprili 16, 2021.
Ndege ya upelelezi ya kikosi cha anga cha Marekani RC-135 ikiruka juu ya Bahari ya Pasifiki karibu na pwani ya Kamchatka Aprili 16, 2021. via REUTERS - RUSSIAN DEFENCE MINISTRY
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Urusi limetuma haraka ndege ya kivita aina ya MiG-31 ili kusindikiza ndege ya upelelezi ya Marekani iliyokuwa ikiruka juu ya bahari ya Pasifiki na kukaribia mpaka wa Urusi, kulingana na taarifa kutoka kwa kikosi cha wanamaji cha Utusi, ikinukuliwa na shirika la habari la Interfax.

Ndege hiyo ya kivita aina ya Mig ilirejea katika kituo chake baada ya ndege ya kijeshi ya Maekani-Boeing RC-135 kuondoka karibu na mpaka wa Urusi, kulingana na chanzo cha kijeshi kutoka Urusi.

Kwa upande wake, Marekani ilituma ndege za kivita kusindikiza ndege ya kikosi cha wanamaji cha Urusi Tupolev Tu-142 ambayo imekuwa ikiruka kwenye bahari ya Pasifiki, Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema, ikinukuliwa na shiriak la habari la RIA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.