Pata taarifa kuu
MAREKANI-CHINA-USHIRIKINAO

Marekani yaamua kufunga ubalozi wake mdogo wa Chengdu nchini China

Marekani imelazimika kufunga ubalozi wake mdogo wa Chengdu nchini China, baada ya Beijing kuumuru ubalozi huo kufungwa. Hatu hii ilikuja siku chache baada ya Washington kuamuru ubalozi mdogo wa China huko Houston kufungwa.

Afisa wa polisi wa China asimama nje ya ubalozi mdogo wa zamani wa Marekani huko Chengdu, katika Jimbo la Sichuan, kufuatia baada ya maafisa wa ubalozi huo kuondoka Julai 27, 2020.
Afisa wa polisi wa China asimama nje ya ubalozi mdogo wa zamani wa Marekani huko Chengdu, katika Jimbo la Sichuan, kufuatia baada ya maafisa wa ubalozi huo kuondoka Julai 27, 2020. REUTERS/Thomas Peter
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo alisema kuwa serikali ya Marekani mjini Washington iliamua kuchukua hatua hiyo kwasababu Beijing ilikua ''inaiba'' akili miliki.

Wakati huo huo Msemaji wa wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin alijibu akisema hatua ya Marekani ni "mkanganyiko wa uongo wa chuki dhidi ya China".

Makumi kadhaa ya polisi wa China wamekuwa wakipelekwa nje ya ubalozi huo, wakiwataka watu waliokusanyika nje kushuhudia kinachoendelea kuondoka na kujaribu kuzuia vitendo vya uchokozi

Baada ya muda wa mwisho uliowekwa wa saa 72 kwa wanadiplomasia wa China kuwa wameondoka Houston kumalizika Ijumaa, taarifa zinasema wanaume walionekana kuwa ni maafisa wa Marekani walifungua kwa nguvu mlango ili kuingia ndani ya ubalozi huo.

Hali ya wasiwasi imekua ikiongezeka kati ya nchi hizo mbili zenye nguvu za nyuklia juu ya masuala mbalimbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.