Pata taarifa kuu
CHINA-MAREKANI-USHIRIKIANO

China yaamuru ubalozi mdogo wa Marekani huko Chengdu kufungwa

Siku tatu baada ya uamuzi wa Washington kufunga ubalozi mdogo wa China huko Houston, Beijing imeamuru kufungwa kwa ubalozi mdogo wa Marekani katika mji wa Chengdu, Kusini Magharibi mwa China.

Lango la ubalozi mdogo wa Marekani katika mji wa China wa Chengdu, Sichuan, Julai 23, 2020.
Lango la ubalozi mdogo wa Marekani katika mji wa China wa Chengdu, Sichuan, Julai 23, 2020. GOH Chai Hin / AFP
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu ni "jibu halali na la lazima kwa hatua zisizo na maana za Marekani", Wizara ya Mambo ya Jje ya China imesema katika taarifa.

Awali China ililaani vikali uamuzi huo waMarekani na kutishia kuchukua hatua za kulipiza kisasi.

"Hatua ya Marekani kufunga ubalozi wa China huko Houston, bila hata hivyo kuishirikisha serikali ya Beijing, katika kipindi kifupi kama hiki ni muendelezo wa hatua za hivi karibuni za Marekani dhidi ya China," alisema msemaji wa wizara ya mambo ya Nje ya China, Wang Wenbin.

Akiwa ziarani jijini London Jumanne, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo, alitoa wito Jumanne kwa kuunda muungano wa kimataifa ili kuzuia "tishio" alilodai kutoka China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.