Pata taarifa kuu
MAREKANI-CHINA-HUAWEI-USHIRIKINAO-BIASHARA

Washington yaweka vikwazo dhidi ya wafanyakazi wa Huawei

Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya wafanyakazi wa kampuni kubwa ya simu kutoka China ya Huawei, hatua ambayo inaendelea kuzidisha shinikizo zaidi kwa China, ambayo ilimwitisha balozi wa Marekani jijini Beijing.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo mbele ya nembo ya Huawei katika mkutano na waandishi wa habari Julai 15, 2020.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo mbele ya nembo ya Huawei katika mkutano na waandishi wa habari Julai 15, 2020. AFP
Matangazo ya kibiashara

Mvutano kati ya nchi hizi mbili zenye kustawi kuchumi zaidi duniani wa umeongezeka katika nyanja mbalimbali, baada ya China kuweka sheria ya usalama wa kitaifa kwa Hong Kong mwishoni mwa mwezi Juni, na China kudai kuwa sehemu yake ardhi, eneo la bahari Kusini mwa China, bila kusahau ukandamizaji wa China dhidi ya Waislamu wa Uighur huko Xinjiang, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Wiki hii Rais wa Marekani Donald Trump alitia saini sheria inayoagiza nchi hiyo kulitambua eneo la Hong Kong kama la upendeleo, hatua inayokuja baada ya China kupitisha sheria mpya za usalama kuhusu eneo hilo.

Hatua hii ya Marekani imeikasirisha China ambayo imesema italipiza kisasi dhidi ya hatua hiyo ya Trump, itakayoruhusu pia mabenki kuwekewa vikwazo kuhusiana na hatua yake dhidi ya Hong Kong.

Uhusiano kati ya Marekani na China umekuwa mbaya zaidi, tangu mataifa hayo mawili yaliposaini awamu ya kwanza ya makubaliano ya biashara lakini hadi sasa mazungumzo hayo yamekwama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.