Pata taarifa kuu
CHINA-MAREKANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Vyombo vya habari vya China vyashutumu Washington kwa 'Propaganda'

Gazeti moja lililo na uhusiano wa karibu na Chama cha Kikomunisti nchini China (CCP) limeishtumu kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo, ambaye alihakikishia saa chache kabla kuwa ana "ushahidi wa kutosha" unaoonyesha kuwa ugonjwa wa Covid-19 ulitokea katika maabara ya China.

Waziri wa Mambo ya Nje aw Marekani Mike Pompeo, hapa, ilikuwa katika mkutano na waandishi wa habari, Washington, Aprili 29, 2020
Waziri wa Mambo ya Nje aw Marekani Mike Pompeo, hapa, ilikuwa katika mkutano na waandishi wa habari, Washington, Aprili 29, 2020 Andrew Harnik/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Gazeti la Global Times limeitaja kauli hiyo kuwa ni uzushi na habari zisizokuwa na msingi wowote.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani hana uthibitisho wowote kwamba virusi vya Corona vilitokea katika maabara ya Wuhan, limeandika Gazeti la Global Times, na kuitaka Marekani kutoa vithibitisho ambavyo wawakilishi wake wametangaza."

Utawala wa Trump unaendelea na vita vya propaganda visivyo kuwa na faida yoyote, huku ikijaribu kuzuia juhudi za mataifa mbalimbali katika mapambano dhidi ya janga la Covid-19," Gazeti hilo limeongeza kwa lugha ya Kiingereza.

Akiongea kwenye runinga ya ABC siku ya Jumapili, Mike Pompeo alitangaza kuhusu virusi hivyo vya Corona kwamba "kuna ushahidi wa kutosha kwamba vilitengenezwa na maabara huko Wuhan."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.