Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-CORONA-AFYA-UCHUMI

Donald Trump: Virusi vya Corona vilitengenezwa katika maabara ya China

Rais wa Marekani Donald Trump amesema ameona ushahidi unaonesha kuwa virusi vya Corona vilitengezwa katika maabara mjini Wuhan nchini China.

Rais wa Marekani, Donald Trump alizungumza kutoka ofisi ndogo ya White House huko Washington, Aprili 30, 2020.
Rais wa Marekani, Donald Trump alizungumza kutoka ofisi ndogo ya White House huko Washington, Aprili 30, 2020. Carlos Barria/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Trump ameendelea kuishtumu China kwa kutofanya vya kutosha kuzuia maambukizi hayo ambayo yamesabisha zaidi ya Wamerakani Milioni 30 kukosa ajira.

Trump mwenyewe ameendelea kukosolewa nchini mwake kwa namna anavyokabiliana na mlipuko huo nchini mwake.

Hivi karibuni rais Donald Trump alilishukia Shirika la Afya Duniani, WHO, na kulilaumu kwa kuegemea upande wa China. Trump alisema asasi hiyo ya kimataifa ilishirikiana na China kuficha ukweli. 

Hata hivyo alitangaza kusitisha ufadhili wa nchi yake kwa shirika hilo la kimataifa. Uamuzi wake huo ulikosolewa vikali, huku mlipuko wa virusi hivyo ukiendelea kuathiri maeneo mengi.

Marekani ndio mfadhili mkubwa wa WHO' anayetoa ufadhili wa kiasi cha dola milioni 400 ambayo ni 15% ya bajeti yake ya mwaka jana.

China ilichangia mwaka 2018-19 karibu dola milioni 76, na yapata dola milioni 10 katika ufadhili, kwa mujibu wa mtandao wa Shirika la Afya Duniani.

Shirika hilo lilitenga kiasi cha dola milioni 675 kukabiliana na magonjwa ya mlipuko na liliripotiwa kuwa litaongeza fedha hizo hadi karibu dola bilioni moja.

Marekani ina idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.