Pata taarifa kuu
MAREKANI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Washington: Remdesivir ni dawa inayosaidia wagonjwa wa Corona kupona haraka

Watafiti wa dawa nchini Marekani wanasema kuna habar njema baada ya kupatikana kwa  dawa ya majaribio ambayo imeonekana kutibu virusi vya Corona.

"Hii inaonyesha kwamba tunaweza kuzuia virusi," amesema Dk. Anthony Fauci kutoka Ofisi ya ndogo ya White House Aprili 29, 2020.
"Hii inaonyesha kwamba tunaweza kuzuia virusi," amesema Dk. Anthony Fauci kutoka Ofisi ya ndogo ya White House Aprili 29, 2020. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Dawa hiyo ya majaribio iliyopewa jina la Remdesivir, inaelezwa kuwa itawasaidia wagonjwa walioambukizwa Corona kupona haraka, lakini bado utafiti zaidi unafanyika.

Dawa ya Remdesivir inapunguza muda wa dalili kutoka siku 15 hadi siku 11 kulingana na majaribio yaliofanywa katika hospitali katika maeneo mbalimbali duniani.

Remdesivir mara ya kwanza ilitengenezwa kutibu ugonjwa wa Ebola. Ni dawa ya kukabiliana na virusi na inafanya kazi kwa kushambulia enzymes ambazo virusi vinahitaji ili kuweza kuzaana ndani ya seli ya mwili wa mwanadamu.

Anthony Fauci, ambaye ni mmoja wa wadau muhimu katika jopo kazi la kupambana na mamabukizi ya Corona nchini Marekani, NIAID, amesema Remdesivir inaweza kupunguza dalili na kusaidia mtu kupona kwa haraka..

Marekani ina mamabukizi ya watu Milioni 1 na wengine zaidi ya Elfu 60 wamepoteza maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.