Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Marekani yakubali mazungumzo na Korea Kaskazini bila masharti

Marekani imesema iko tayari kwa mazungumzo na Korea Kaskazini "bila masharti", ingawa inaendelea kutathmini njia zote, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kutumia nguvu za kijeshi, ili Pyongyang iachane na mpango wake wa silaha za nyuklia.

Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson.
Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson. REUTERS/Alex Brandon/Pool
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo ambapo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson, alikuwa akitoa tangazo hilo ambalo linaonyesha jinsi gani Marekani imeanza kulegeza msimamo wake, Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un ameendelea kuongeza vita vya maneno katika miezi ya hivi karibuni, akionyesha nia yake ya kuifanya nchi yake kuwa yenye "nguvu kubwa za nyuklia na kijeshi duniani".

Hata hivyo hali hiyo haikatazi Pyongyang "kukubali kuwa ni muhimu kuepuka vita na Marekani," amesema Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Mambo ya Kisiasa, Jeffrey Feltman, ambaye ni raia wa Marekani.

Afisa huyo mwandamizi wa Umoja wa Mataifa alielezea siku ya Jumanne katika kikao cha faragha cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ziara yake wiki iliyopita nchini Korea ya Kaskazini, ambapo Pyongyang ilishutumu Marekani kutaka kuanzisha vita na Korea Kaskazini".

Mpaka sasa, utawala wa Donald Trump umekua ukisema kuwa uwezekano wa mazungumzo na Korea ya Kaskazini hayawezi kufanyika kwa muda mrefu kwa sharti ya kupokonywa silaha za nyuklia.

"Sio sahihi kusema" tutazungumza nanyi ikiwa mtakuja kwenye meza ya mazungumzo mkiwa tayari kuacha mpango wenu wa nyuklia, "alisema Tillerson siku ya Jumanne katika mkutano mjini Washington. "Wamewekeza kiasi kikubwa katika sekta hiyo," Bw Tillerson alisema kuhusu suala la maendeleo ya makombora ya masafa marefu yanayokwenda hadi bara jingine na silaha za nyuklia vinavyotengenezwa na Korea Kaskazini.

"Tuko tayari kuzungumza kwa wakati wowote Korea ya Kaskazini itakua tayari kuzungumza," alisema. "Tuko tayari kufanya mkutano wa kwanza bila masharti".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.