Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KASKAZINI-KOREA KUSINI-USALAMA

Marekani na Korea Kusini wazindua mazoezi makubwa ya kijeshi ya angani

Marekani na Korea Kusini zimeanzisha leo Jumatatu mazoezi makubwa ya kijeshi ya angani, hatua ambayo Korea Kaskazini imeshutumu na kusema kwamba ni kutaka kuchochea vita vya kinyuklia wakati wowote.

Majeshi ya Kora Kusini na yale ya Marekani mara kwa mara wanafanya mazoezi ya kijeshi ya pamoja. Hapa ilikua Aprili 26, 2017  Pocheon.
Majeshi ya Kora Kusini na yale ya Marekani mara kwa mara wanafanya mazoezi ya kijeshi ya pamoja. Hapa ilikua Aprili 26, 2017 Pocheon. JUNG Yeon-Je / AFP
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Washington mshauri wa rais kuhusu masuala ya kiusalama katika ikulu ya rais nchini Marekani ameonya kuwa kuna uwezekano wakuzuka vita dhidi ya Korea Kaskazini, siku moja baada ya Pyongyang kurusha makombora ya masafa marefu ambayo inaripotiwa kuwa yana uwezo wa kufika Marekani.

Mazoezi ya kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini yameanza leo na yatadumu siku tano huku yakijumuisha ndege 230 za kijeshi.

Korea Kaskazini imelaani mapema operesheni hiyo,huku ikishtumu utawala wa rais wa Donald Trump kuwa "unataka vita vya nyuklia kwa njia zote."

Aina hii ya mazoezi imezua hasira kwa upande wa Pyongyang ambayo inayachukulia kama uvamizi wa eneo lake. Mvutano unaendelea wakati ambapo Korea Kaskaziniikiendelea na majaribio yake ya makombora ya masafa marefu.

Mazoezi haya ya pamoja kati ya majeshi ya Marekani na Korea Kusini yanafanyika siku tano baada Korea Kaskazini kufanya jaribio lake jipya la kombora la masafa marefu lenye uwezo wa kuwenda hadi bara jingine (ICBM), na katika sehemu yoyote nchini Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.