Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI-USALAMA

Pyongyang: Vitisho vya Marekani vinaweza kusababisha vita

Mazoezi ya pamoja ya kijeshi yanayoendeshwa na majeshi ya Marekani na Kusini Korea ambayo ni vitisho vya vita kutoka Washington yatasababisha kulipuka kwa vita katika rasi ya Korea, wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini.

Kiongozi wa Korea KAskazini Kim Jong-un akijadiliana na maafisa waandamizi wa jeshi la nchi hiyo.
Kiongozi wa Korea KAskazini Kim Jong-un akijadiliana na maafisa waandamizi wa jeshi la nchi hiyo. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Swali pekee ambalo linasalia ni kujua lini vita hivyo vitalipuka, "msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini ameongeza katika taarifa iliyorejelewa na shirika la habari la KCNA la Korea Kaskazini.

"Hatutaki vita lakini hatutasita kujihami, na kama Marekani itatumia uvumilivu wetu kuanzisha vita vya nyuklia, tutamfundisha adabu kupitia nguvu zetu za nyuklia, ambazo tumeimarisha kwa ustadi wa hali ya juu, "amesema.

Korea Kusini na Marekani, siku ya Jumatatu Desemba 4 walizindua mazoezi makubwa ya pamoja ya angani, wiki moja baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio jingine la kombora ya masafa marefu. hali ambayo ilizua hali ya sintoifahamu katika kanda rasi ya Korea.

Kwa mujibu wa afisa mmoja, mazoezi ya kila mwaka ya Marekani na Korea Kusini, yanayojulikana kama "Ace Vigilant", yatamalizika kesho Ijumaa.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa White House, HR McMaster, alibaini kwamba uwezekano wa vita dhidi ya Korea Kaskazini "umekua ukiongezeka kila kukicha" na Seneta kutoka chama cha Republican Lindsey Graham aliomba siku ya Jumapili kwa uongozi wa jeshi la Marekani Pentagon kurejesha familia za askari wa Marekani zilizotumiwa nchini Korea Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.