Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-JAPAN-USALAMA

Mbio za mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini katika tarehe chache muhimu

Kwa mara ya pili ndani ya muda usiyozidi mwezi mmoja, Korea ya Kaskazini ilifyatua kombora Ijumaa hii kupitia anga ya Japan, kombora ambalo lilifikia umbali usio wa kawaida.

Mjini Seoul  Septemba 15, 2017, mbele ya televisheni ikitangaza jaribio jipya laa kombora lililorushwa na Korea Kaskazinikupitia anga ya Japan.
Mjini Seoul Septemba 15, 2017, mbele ya televisheni ikitangaza jaribio jipya laa kombora lililorushwa na Korea Kaskazinikupitia anga ya Japan. REUTERS/Kim Hong-Ji
Matangazo ya kibiashara

Hatua muhimu ya mipango ya nyuklia na majaribio ya makombora ya masafa marefuya Kaskazini:

- Mwanzo, mwishoni mwa miaka ya 1970 -

Korea Kaskazini ilianza kufanya kazi mwishoni mwa miaka ya 1970 kuhusu toleo la kombora la Sovieti Scud-B (linalokwenda umbali wa kilomita 300), kwa jaribio la kwanza mwaka 1984.

Kati ya mwaka 1987 na 1992, Pyongyang iliftengeneza makombora yamasafa marefu, ikiwa ni pamoja na Taepodong-1 (linalokwenda umbali wa kilomita 2,500) na Taepodong-2 (linalokwenda umbali wa kilomita 6,700).

Mnamo mwaka 1989, picha za satellite za Marekani ziliffichua kuwepo kwa kituo cha nyuklia katika mji wa Yongbyon, kaskazini mwa Pyongyang.

1994: makubaliano na Washington -

Mnamo mwezi Oktoba 1994, makubaliano ya nchi mbili kati ya Marekani na Korea Kaskazini, ambayo yaliahidi kuvunja mpango wake wa nyuklia badala yake kuruhusiwa ujenzi wa mitambo ya vifaa vya kiraia. Mkataba huo ulikuja miezi mitatu baada ya kifo cha Kim Il-Sung, na nafasi yake kuchukuliwa na mwanawe, Kim Jong-Il.

Mwishoni mwa mwaka 2002, Washington iliishtaki Pyongyang kwa kufanya mpango wa siri wenye utajiri wa uranium. Korea Kaskazini iliwafukuza wakaguzi kutoka Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) na kisha kujitoa katika Mkataba dhidi ya Nyukliaji (NPT).

- 2006: jaribio la kwanza -

Mnamo Machi 2005, Pyongyang ilikamilisha kusitishwa kwa makombora ya masafa marefu na tarehe 9 Oktoba 2006, ilifanya jaribio lake la nyuklia la kwanza.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipiga kura kwa vikwazo vya kiuchumi na biashara, ambavyo viliongezwa na kuimarishwa mara kadhaa.

Mnamo mwezi Februari 2007, Pyongyang ilikubali kufuta mpango wake wa nyuklia na kuwapokea wakaguzi wa IAEA badala yake kupewa tani milioni moja ya mafuta na kutolewa kwenye orodha ya Washington ya nchi za kigaidi.

- 2009: kuvunjikwa kwa mkataba kufuatia jaribio la pili -

Mnamo mwezi Aprili 2009, Pyongyang ilijitoa kwenye mazungumzo ya sita (Korea mbili, China, Russia, Marekani, Japan) yalioanza mwezi Agosti 2003 na kisha kuimarisha mpango wake wa nyuklia. Mei 25, jaribio la nyuklia la pili la ardhini lilifanyika.

Mnamo mwezi Desemba 2011, Kim Jong-Un alimrithi baba yake. Uchunguzi wa nyuklia wa tatu ulifanyika mnamo mwezi Februari 2013.

- 2016: mvutano -

Januari 6, kulifanyika jaribio la nyuklia la ardhini. Korea Kaskazini inasema kuwa ilijaribu bomu la hidrojeni, ambalo lilishtumiwa na wataalam.

Mnamo mwezi Agosti, kwa mara ya kwanza, Korea Kaskazini ilirusha kombora moja kwa moja kwenye eneo la kiuchumi la bahari ya Japan. Tarehe 9 Septemba, serikali ililitangaza kwamba walifanya jaribio lao la tanu la nyuklia.

- 2017: Majaribio kadhaa yashuhudiwa

Mnamo mwezi Julai, Korea Kaskazini ilifyatua makombora mawili ya yanayoweza shambulia bara jingine (ICBM) ambayo yalionekana kuwa yanaweza kufika hadi bara la Amerika.

Rais wa Marekani Donald Trump aliatishia "kuishambulia" Korea Kaskazini, tarehe 29 Agosti Pyonyang ilijibu kwa kufyatua kombora la masafa marefu kupitia anga ya Japan.

Septemba 3, jaribio la sita la nyukilia, lenye nguvu zaidi na ambalo kwa mujibu wa serikali ay Korea Kaskazini lilihusisha bomu la Hidrojene ndogo kwa kuandaa kombora.

Tarehe 15 Septemba, ndani ya muda usiozidi wiki moja baada ya Umoja wa Mataifa kupitisha vikwazo vya nane, Pyongyang ilirusha kombora jingine kupitia anga ya Japan kwenye umbali wa kilomita 3,700, kwa mujibu wa serikali ya Seoul.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.