Pata taarifa kuu

Mexico yasitisha uhusiano wake kidiplomasia na Ecuador

Nairobi – Mexico imetangaza kusitisha uhusiano wake wa kidiplomasia na nchi ya Ecuador baada ya polisi kuvamia ubalozi wa Mexico mjini Quito wakiwa na lengo la kumkamata makamu wa Rais wa zamani wa Ecuador Jorge Glas.

Police and military officials walk outside the Mexican embassy from where they forcibly removed the former Ecuador Vice President Jorge Glas in Quito, Ecuador April 5, 2024. REUTERS/Karen Toro
Mexico ilisema ilitoa kibali kwa Glas kuishi nchini humo baada ya kuchunguza kwa udani hali aliokuwa anakabiliwa nayo REUTERS - Karen Toro
Matangazo ya kibiashara

Glas alitorokea katika ubalozi huo mwezi Desemba mwaka wa 2023 baada ya Ecuador kutoa hati ya kukamatwa kwake akidaiwa kuhusika na ufisadi.

Kwa mujibu wa wakili wa Glas aliyehudumu katika wadhifa wa makamu wa rais wa Ecuador kati ya 2013 na 2017, kiongozi huyo wa zamani hana hatia.

Makamu huyo wa rais wa zamani aliondolewa katika wadhifa wake kutokana na madai ya kujihusisha na ufisadi akiwa afisa wa umma.

Alihukumiwa kifungo cha miaka sita jela baada ya kuondolewa afisini kwa kuhusishwa na ufisadi katika kampuni kubwa ya ujenzi ya Brazil Odebrecht.

Mexico siku ya Ijumaa ililalamikia kile ilichosema ni uwepo wa maofisa wa polisi wa Ecuador katika ubalozi wake nchini humo.
Mexico siku ya Ijumaa ililalamikia kile ilichosema ni uwepo wa maofisa wa polisi wa Ecuador katika ubalozi wake nchini humo. REUTERS - Karen Toro

Kwa mujibu wa taarifa ya waendesha mashtaka, kiongozi huyo wa zamani alipokea Dolla Milioni 13.5 kama hongo.

Aliachiwa kutoka gerezani Novemba mwaka jana lakini mamlaka ya Ecuador ikatoa hati nyingine ya kukamatwa kwa tuhuma zaidi ya rushwa, hali iliompekea kutafuta kumfanya hifadhi katika ubalozi wa Mexico.

Mexico ilisema ilitoa kibali kwa Glas kuishi nchini humo baada ya kuchunguza kwa udani hali aliokuwa anakabiliwa nayo.

Hatua hii inakuja baada ya siku ya Ijumaa, mamlaka nchini Morocco kulalamikia kile ilichosema ni unyanyasaji kutokana na uwepo wa maofisa wa polisi katika ubalozi wake wa Quito.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.