Pata taarifa kuu

Kremlin: Maoni ya Biden ya kumuita Putin "mnyanyasaji" 'haikubaliki'

Moscow imesema matamshi ya rais wa Marekani Joe Biden kuhusu mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, aliyemwita kama "dhalimu", wakati wa hotuba yake kwa taifa,"hayakubaliki. Kwa mara ya pili katika muhula wake, Joe Biden alihutubia wananchi wake kutoka ofisi ya Oval. Hotuba iliyotangazwa kuwa kuu na Ikulu ya White House.

Dmitry Peskov, msemaji wa Kremlin, huko Moscow, Mei 25, 2023.
Dmitry Peskov, msemaji wa Kremlin, huko Moscow, Mei 25, 2023. © AFP - MIKHAIL METZEL
Matangazo ya kibiashara

 

Na mwanahabari wetu huko Washington, Guillaume Naudin

Kremlin inasema matamshi ya rais wa Marekani Joe Biden ambapo aliifananisha Urusi na Hamas na kumwita Vladimir Putin kuwa "mnyanyasaji" "hayakubaliki".

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema: "Hatukubali sauti kama hiyo kuhusiana na Shirikisho la Urusi, kuhusiana na rais wetu.

Alisema "maneno kama haya hayafai kwa viongozi wanaowajibika wa majimbo, na ni vigumu kukubalika kwetu".

Joe Biden pia amesisitiza kuwa Hamas haiwawakilishi Wapalestina, ambao pia wana haki ya kuishi kwa amani na usalama, kama majirani zao wa Israel. Kwa mara nyingine tena amewataka Waisrael wajizuiwe na hasira zao na kuheshimu sheria za kibinadamu katika kukabiliana na Hamas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.