Pata taarifa kuu

Misaada ya kibinadamu yapaswa kuja hivi karibuni kusaidia Gaza iliyozingirwa

Misaada ya kibinadamu inapaswa kuanza kuingia Gaza Alhamisi hii tarehe 19 jioni au siku Ijumaa, rais wa Marekani Joe Biden ametaka kumhakikishia binafsi rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi. Huko Rafah, magari makubwa ya mizigo yaliyosheheni misaada yako tayari kusaidia wakaazi wa Gaza.

Katika kusubiri kufunguliwa kwa kivuko cha Rafah, katika mji wa Al-Arish katika Peninsula ya Sinai nchini Misri, Oktoba 15, 2023.
Katika kusubiri kufunguliwa kwa kivuko cha Rafah, katika mji wa Al-Arish katika Peninsula ya Sinai nchini Misri, Oktoba 15, 2023. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Waandishi wa habari tu kutoka vyombo vya habari vya serikali na visivyo vya serikali kutoka Misri pamoja na wale wa idhaa za Kiarabu na "marafiki" ndio wanaokubaliwa kwa sasa kwenye mpaka na Gaza. Waandishi wengine wote wa habari wamerejeshwa nyuma na vizuizi kadhaa vya usalama vinavyoanzia Mfereji wa Suez Magharibi hadi Gaza Mashariki. Hii imekuwa hivyo kwa miaka kadhaa, lakini leo hatua ni mbaya zaidi kuliko hapo awali.

Israel inaendelea kuushambulia kwa makombora Ukanda wa Gaza, ambako Wapalestina milioni 2.4 wanaishi ambao wakati mwingine wakihitaji mahitaji ya kimsingi. Na Gaza inahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu, amekumbusha mjumbe wetu maalum huko Jerusalem, Guilhem Delteil. Waziri wa Ulinzi wa Israel ametangaza kwamba alikuwa akitekeleza hatua ya "kuzingirwa" kwa eneo hilo, na kusitisha usambazaji wa umeme, maji na bidhaa zote kwenye eneo la Palestina. Kiwanda pekee cha umeme kimefungwa kwa wiki moja. Upatikanaji wa maji na chakula ni mgumu. Shirika la Afya duniani linabaini kwamba "janga la kibinadamu" linatishia wakaazi wa Gaza.

Ishara ya kutokuwa na subira kwa wakazi wa Gaza, dazeni chache za wakaazi wamekusanyika asubuhi ya leo mbele ya kituo cha mpakani cha Rafah kwa matumaini ya kuweza kuondoka. Lakini kulingana na Joe Biden, makubaliano hayo yanahusu kuingia kwa malori ndani ya eneo hilo. Wapalestina wasiruhusiwe kuondoka. Na rais wa Marekani alionya: katika tukio la matumizi mabaya ya misaada na Hamas, kivuko cha mpaka kitafungwa tena.

Zaidi ya tani elfu moja za misaada

Takriban magari mia moja ya mizigo mizito kutoka Misri yakiwa yamepakia misaada ya kibinadamu kutoka Bonde la Nile yamekuwa yakisubiri tangu Jumatano mbele ya lango la kivuko cha Rafah, anaripoti mwandishi wetu mjini Cairo, Alexandre Buccianti.

Wanasubiri vifaa vya ujenzi vilivyotumwa kutoka Misri ili kumaliza kukarabati mahali pa kuvuka upande wa Palestina. Kituo hicho kimepunguzwa kuwa miamba mikubwa ya mchanga kutokana na milipuko kadhaa ya Israel. Kabla ya kupita, lori hizo lazima pia zipate idhni kutoka kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayosimamia wakimbizi ambao wenyewe walipaswa kupata idhini kutoka kwa mamlaka ya usalama ya Israeli.

Mbali na misaada ya Misri, zaidi ya tani elfu moja za bidhaa za matibabu, mahema, blanketi na vyakula kutoka nchi za Kiarabu na za Kiislamu, lakini pia kutoka maeneo mengine duniani zimewasili katika siku za hivi karibuni katika uwanja wa ndege wa Al-Arich ulioko karibu kilomita hamsini kutoka Gaza. Malori ya kubebea mafuta pia yatahitajika kusambaza jenereta za hospitali za Gaza pamoja na maji ya kunywa.

Wizara ya Hali ya Dharura ya Urusi ilitangaza mnamo Oktoba 19 kwamba Urusi "hivi karibuni" itawasilisha tani 27 za misaada ya kibinadamu kwa raia katika Ukanda wa Gaza. Gari aina ya Ilyushin 76 ikiwa imesheheni unga, sukari na tambi inaripotiwa kuwa njiani kuelekea Misri. Msaada wa Urusi umepangwa kuwasili kwenye Gaza kupitia wawakilishi wa shirika la Hilali Nyekundu ya Misri.

Wapalestina waliokwama huko Gaza wanasubiri kwa hamu lori hizi za misaada ya kibinadamu, katika siku ya 13 ya vita vya kutisha ambavyo vinaendelea, licha ya shughuli kubwa za kidiplomasia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.