Pata taarifa kuu

Canada yaidhinisha kulipuliwa kwa kitu kisichojulikana juu ya anga yake

Ndege ya kivita ya Marekani ilitungua kitu ambacho hakikujulikana nchini Canada Jumamosi mchana, kwa agizo la Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, kuashiria tukio jipya katika anga ya Amerika Kaskazini tangu kuangushwa kwa puto lililodaiwa kuwa la kijasusi la China wiki iliyopita.

Ndege ya kivita ya Lockheed F-22 Raptor.
Ndege ya kivita ya Lockheed F-22 Raptor. (Photo : AFP)
Matangazo ya kibiashara

 

Justin Trudeau alitangaza Jumamosi kwamba "kitu kisichojulikana" kilidunguliwa kilipokuwa kikiruka kaskazini-magharibi mwa nchi, siku moja baada ya Marekani kuharibu puto juu anga ya Alaska. "Nimegiza kulipuliwa kwa kitu kisichojulikana ambacho kilikiuka anga ya Canada," Justin Trudeau aliandika kwenye mtandao wa Twitter. "Ndege kutoka Canada na Marekani zilitumwa kwenye eneo la tukio, na ndege ya Marekani ya F-22 ilifyatua" kombora la AIM 9X na "kuharibu"kitu hicho.

Rais wa Marekani Joe Biden alikuwa ameidhinisha ndege hiyo, mojawapo ya ndege ya Kamandi ya Ulinzi wa Anga ya Kaskazini (NORAD), "kufanya kushirikiana na Canada", ameeleza msemaji wa Pentagon, Pat Ryder.

Vikosi vya Canada "sasa vitapata nafuu na kutathmini mabaki ya kitu hicho," aliongeza Waziri Mkuu wa Canada.

Kitu hicho kilikuwa kikiruka kwa urefu wa mita 12,200, alieleza kwa kina Waziri wa Ulinzi wa Canada, Anita Anand, wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jumamosi jioni, na kilitunguliwa kilomita 160 kutoka mpaka wa Canada na Marekani saa mbili  na dakika 40 jioni.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.