Pata taarifa kuu

Puto lingine ambalo halikutajwa hapo awali laruka juu ya anga ya Colombia

Colombia ilitangaza wikendi hii kwamba puto lingine linaloshukiwa kuwa la China  lililonekana juu ya anga yake, baada ya tahadhari ya Ijumaa Februari 3 kutoka Marekani juu ya 'puto la kijasusi la China' lililoonekana kwenye juu ya anga ya Amerika ya Kusini. 

Pentagon inafuatilia puto la kijasusi la China likiruka juu ya anga la Marekani mnamo Februari 2, 2023.
Pentagon inafuatilia puto la kijasusi la China likiruka juu ya anga la Marekani mnamo Februari 2, 2023. © AP/Larry Mayer
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Wanahewa la Colombia lilisema puto hilo liligunduliwa siku ya Ijumaa asubuhi na kufuatiliwa hadi lilipoondoka kwenye anga yake, na kuhakikisha kwamba wakati wowote "haijatishia" usalama na ulinzi wa nchi.

Mnamo Februari 3, 'mfumo wa kitaifa wa ulinzi wa anga uligundua kitu kilichokuwa juu ya futi 55,000, ambacho kiliingia kwenye anga ya Colombia kupitia eneo la kaskazini mwa nchi, kikienda kwa kasi ya wastani ya noti 25 na kuwa na dadili ya puto," jeshi lilisema katika taarifa siku ya Jumamosi.

Jeshi la Wanahewa la Colombia liliongeza kuwa lilikuwa likifanya "uthibitishaji na nchi na taasisi tofauti ili kujua asili ya kitu hicho".

Siku ya Ijumaa, Pentagon ilisema puto la pili la kijasusi la China lilionekana likiruka juu ya anga ya Amerika ya Kusini, siku moja baada ya puto kama hilo kuguduliwa juu ya anga ya Marekani.

Hakukuwa na maelezo kuhusu kuonekana kwa puto hili ya pili au mwelekeo wake.

Jeshi la Marekani siku ya Jumamosi, kwa agizo la Rais Joe Biden, lilitungua puto la China lililokuwa likiruka juu ya anga ya Marekani, na hivyo kusababisha ukosoaji mkubwa kutoka Beijing.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.