Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Joe Biden: Marekani 'itachukua hatua' ikiwa China 'itatishia uhuru wake'

Marekani 'itachukua hatua' ikiwa China itatishia mamlaka yake, Joe Biden amliahidi Jumanne, Februari 7, wakati uhusiano kati ya Washington na Beijing umezorota katika siku za hivi karibuni kutokana na puto ya China kuonekana juu ya anga ya Marekani, kabla ya kuangushwa baharini.

Wakati wa hotuba yake ya kila mwaka kwa Bunge kuhusu umoja, rais wa Marekani aliahidi kuchukua hatua ikiwa China itatishia Washington, "kama tulivyoonyesha wiki iliyopita."
Wakati wa hotuba yake ya kila mwaka kwa Bunge kuhusu umoja, rais wa Marekani aliahidi kuchukua hatua ikiwa China itatishia Washington, "kama tulivyoonyesha wiki iliyopita." AP - Jim Lo Scalzo
Matangazo ya kibiashara

"Kama tulivyoonyesha wiki iliyopita, ikiwa China itatishia uhuru wetu, tutachukua hatua kulinda nchi yetu na tumefanya hivyo," rais wa Marekani alisema wakati wa hotuba yake kuhusu Umoja.

Wakati wa hotuba yake ya kila mwaka kwa Bunge kuhusu umoja, rais wa Marekani aliahidi kuchukua hatua ikiwa China itatishia Washington, "kama tulivyoonyesha wiki iliyopita."

Washington imeamua kuiangusha puto la kijasusi la China ambalo lilikuwa likiruka juu ya anga yaMarekani kwa siku kadhaa na ambalo lilikusudiwa kukusanya taarifa nyeti.

Beijing inashikilia kwa upande wake kwamba ilikuwa chombo cha kiraia, ambayo ilikusudiwa kukusanya data za hali ya hewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.