Pata taarifa kuu

Vita Ukraine: Mazungumzo ya kidiplomasia yanaendelea kati ya Marekani na Urusi

Mistari ya mazungumzo kati ya Washington na Moscow bado iko wazi licha ya vita nchini Ukraine. Hivi ndivyo maafisa wa Marekani na Urusi wanasema, Jumanne, Novemba 8 asubuhi, bila kudhibitisha hali ya mazungumzo haya, wala utambulisho wa maafisa. Kulingana na Gazeti la Wall Street Journal, Jake Sullivan, mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani ndiye ambaye alizungumza mara kadhaa na washirika wa karibu wa Vladimir Putin.

Rais wa Urusi Vladimir Putin (kushoto) na Rais wa Marekani Joe Biden (kulia). Mistari ya mazungumzo kati ya Washington na Moscow bado iko wazi licha ya vita nchini Ukraine.
Rais wa Urusi Vladimir Putin (kushoto) na Rais wa Marekani Joe Biden (kulia). Mistari ya mazungumzo kati ya Washington na Moscow bado iko wazi licha ya vita nchini Ukraine. © Angela Weiss & Alexey Druzhinin/AFP
Matangazo ya kibiashara

Tahadhari inahitajika katika ikulu ya Kremlin kama katika Ikulu ya White House. Lakini, kwa kifupi tu, habari za Gazeti laWall Street Journal zimethibitishwa huko Moscow sawa na huko Washington.

Kulingana na Gazeti hili la Marekani, Jake Sullivan, mmoja wa washauri wa karibu wa Joe Biden, ndiye ambaye amezungumza mara kadhaa katika wiki za hivi karibuni na watu wawili muhimu wenye ukaribu na Vladimir Putin: Yuri Ouchakov, balozi wa zamani wa Washington, na hasa Nikolai Patrushev, Katibu wa Baraza la Usalama la Urusi. Lengo la mazungumzo haya ni kuzuia mzozo wa Ukraine usienee katika nchi zingine, na juu ya yote kuzuia matumizi ya silaha za nyuklia.

Tishio kubwa la nyuklia

Tayari imefahamika kwamba kufuatia matamshi ya vitisho ya Vladimir Putin kuhusu suala la nyuklia mwezi Septemba mwaka huu, Marekani iliionya Urusi kuhusu athari kama hali hiyo itatokea. Lakini kufanyika kwa mazungumzo haya kwa kiwango cha juu namna hii bado habari nyingi hazijavuja. Hii ni ishara ya uzito wa tishio hilo, lakini pia nia ya pande hizo mbili kuendelea kuwasiliana juu ya suala hili hatari kwa bara zima la Ulaya.

"Tunadumisha mawasiliano yaliyolengwa na Marekani kuhusu masuala yanayotokea," amethibitisha Maria Zakharova, msemaji wa diplomasia ya Marekani, Jumanne asubuhi. "Ni kwa manufaa ya Marekani kudumisha mawasiliano" na Kremlin, kwa upande wake amesema Jake Sullivan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.