Pata taarifa kuu

G7 yalaani vikali hatua ya Korea Kaskazini ya kurusha makombora

Kundi la nchi 7 zenye uchumi wa juu duniani, G7, 'zimelaani vikali' hatua ya Korea Kaskazini ya kurusha makombora, siku ya Ijumaa huku kukiwa na ongezeko kubwa la mvutano kwenye rasi ya Korea, na kulaani ukandamizaji wa "kinyama" nchini Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock, wa pili kushoto, akihudhuria kikao cha kwanza cha kazi cha mawaziri wa mambo ya nje wa G7 na mawaziri wenzake Melanie Joly wa Canada, kulia katikati, Yoshimasa Hayashi wa Japan, wa pili kulia, James Cleverly wa Uingereza, katikati kushoto, Josep Borrell wa EU, kulia na Antonio Tajani wa Italia, kushoto, wakati wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa G7 mjini Muenster, Ujerumani, Alhamisi, Novemba 3, 2022.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock, wa pili kushoto, akihudhuria kikao cha kwanza cha kazi cha mawaziri wa mambo ya nje wa G7 na mawaziri wenzake Melanie Joly wa Canada, kulia katikati, Yoshimasa Hayashi wa Japan, wa pili kulia, James Cleverly wa Uingereza, katikati kushoto, Josep Borrell wa EU, kulia na Antonio Tajani wa Italia, kushoto, wakati wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa G7 mjini Muenster, Ujerumani, Alhamisi, Novemba 3, 2022. AP - Wolfgang Rattay
Matangazo ya kibiashara

"Sisi, wanachama wa G7, tunalaani vikali mfululizo haramu na ambao haujawahi kushuhudiwa wa kurusha makombora ya balestiki kutoka Korea Kaskazini, ikiwa ni pamoja na makombora mengi ya kuvuka mabara," imesema taarifa ya mwisho iliyopitishwa baada ya mkutano wa siku mbili wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa kundi la nchi 7 zenye uchumi wa juu duniani, G7, huko Münster, Ujerumani.

Aidha wametoa wito kwa Korea Kaskazini "kusitisha mara moja shughuli yake ya kuhatarisha usalama" na "kuheshimu wajibu wake wa kimataifa".

Pyongyang ilirusha takriban makombora 30 siku ya Jumatano na Alhamisi, likiwemo lililomaliza mkondo wake karibu na eneo la maji ya kusini, kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa Vita vya Korea mwaka 1953. Nchi hiyo pia ilirusha kombora la balestiki la kuvuka mabara (ICBM) Alhamisi asubuh , lakini inaonekana limeshindwa.

"Jaribio lolote la nyuklia au hatua yoyote hatari itakabiliwa na jibu la haraka, thabiti na la umoja", zimeonye nchi za G7.

Aidha, G7 inaeleza katika taarifa hiyo ya mwisho, Ijumaa, kuunga mkono maandamano yanayoendelea nchini Iran, huku ikilaani ukandamizaji wa "kinyama" unaofanywa na mamlaka ya Iran na shughuli ya "kuhatarisha usalama" ya Tehran duniani.

Angalau makombora 23 yarushwa na Korea Kaskazini

"Sisi, wanachama wa G7, tunaelezea kuunga mkono matarajio ya kimsingi ya watu wa Iran kwa siku zijazo ambapo usalama na haki za binadamu zinaheshimiwa na kulindwa", wamebaini, wakilaani "matumizi ya kikatili na ya kupita kiasi ya nguvu" katika ukandamizaji dhidi ya maandamano.

Iran imetikiswa kwa takriban miezi miwili na maandamano yaliyotokana na kifo cha Mahsa Amini mnamo Septemba 16, Mkurdi wa Iran aliyekamatwa siku tatu zilizopita na polisi inayohusika na kushimisha maadili ambayo ilimtuhumu kwa kuvunja kanuni kali ya mavazi ya hijabu, ambayo inawalazimu wanawake na wasichana kuvaa hijabu hadharani. .

Makumi ya watu, hasa waandamanaji lakini pia maafisa wa vikosi vya usalama, wameuawa tangu kuanza kwa maandamano, kulingana na mamlaka. Mamia zaidi, ikiwa ni pamoja na wanawake wengi, walikamatwa.

Hatimaye, mawaziri wa G7 wanalaani "shughuli za kuhatarisha usalama za Iran katika Mashariki ya Kati na kwingineko" ikiwa ni pamoja na usambazaji wa "dege zisizo na rubani au uhamisho wa silaha kwa washirika wa serikali na wasio wa serikali".

Kyiv na nchi za Magharibi zinaishutumu Tehran kwa kuipa Urusi ndege zisizo na rubani katika vita vyake dhidi ya Ukraine, jambo ambalo nchi hizo mbili zinakanusha.

G7 inaleta pamoja Marekani, Kanada, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia na Japan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.