Pata taarifa kuu
UCHAUZI-SIASA

Marekani yafanya uchaguzi wa katikati ya muhula

Ni Siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu nchini Marekani. Wapiga kura wa Marekani wanapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa katikati ya muhula siku ya Jumanne. Ni suala la kuwachaguwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na theluthi moja ya wajumbe wa Bunge la Seneti pamoja na kufanya uchaguzi wa viongozi katika ngazi za mashinani kote nchini.

Atlanta, Georgia, Novemba 8, 2022: Katika ukumbi wa mazoezi kuna vituo vya kupigia kura kwa ajili ya chaguzi hizi za katikati ya muhula nchini Marekani.
Atlanta, Georgia, Novemba 8, 2022: Katika ukumbi wa mazoezi kuna vituo vya kupigia kura kwa ajili ya chaguzi hizi za katikati ya muhula nchini Marekani. REUTERS - JONATHAN ERNST
Matangazo ya kibiashara

Vituo vya kwanza vya kupigia kura vilifunguliwa saa 12 asubuhi kwa saa za ndani kwenye Pwani ya Mashariki, Jumanne ya kwanza kufuatia Jumatatu ya kwanza ya Novemba, kulingana na desturi ya uchaguzi wa kitaifa nchini Marekani. Chaguzi za katikati mwa muhula ambazo zina sifa ya mashindano ya karibu na kuwa ghali zaidi katika historia ya Marekani.

Lakini zaidi ya Wamarekani milioni 42 tayari wamepiga kura mapema, anaripoti mwandishi wetu wa Washington, Guillaume Naudin. Ama kwa njia ya posta, au kwa kuweka kura zao moja kwa moja kwenye masanduku yaliyotolewa kwa madhumuni haya au katika vituo vya kupigia kura vilivyofunguliwa kwa siku kadhaa kulingana na majimbo. Imekuwa tabia na pia ni kitu cha kugombea. Katika angalau majimbo matatu, ikiwa ni pamoja na majimbo muhimu, rufaa imewasilishwa na Chama cha Republican kuomba kwamba baadhi ya kura hizi zisihesabiwe. Upigaji kura wa posta una sifa ya kupendelea Wademocrats.

Baadhi ya Warepublican, ambao bado wanasema uchaguzi wa urais wa 2020 ulikumbwa na udanganyifu, wametangaza kuwa hawatatambua matokeo ikiwa kutaonekana upendeleo. Hii ndio kesi ya Kari Lake, mwandishi wa habari wa zamani wa Fox News kwa miongo miwili, na msemaji wa wanaharakati wanaopinga kporomosha mimba. Anajitokeza kama "Trump katika sketi" anayetarajia kuwa gavana, anaripoti mwandishi wetu maalum huko Phoenix, Thomas Harms. Bado anapinga uchaguzi wa 2020, na hasemi ikiwa atakubali matokeo ya uchaguzi huu wa katikati ya muhula.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.