Pata taarifa kuu

Joto la kisiasa lapanda Marekani siku mbili kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula

Nchini Marekani, kampeni za katikatiti ya muhula, kuwachagua wabunge na baadhi ya Maseneta, zinamalizika leo, kuelekea siku ya mwisho ya kupiga kura siku ya Jumanne.

Rais Joe Biden, anaongoza kampeni ya chama chake cha Democratic mjini Maryland, ambako chama hicho kinatumai kuwa, kitashinda kiti cha Ugavana kutoka kwa chama cha Republican. Naye rais wa zamani Donald Trump, ataongoza kampeni za mwisho katika jimbo la Ohioa, kuwaombea wagombea wa chama cha Republican.
Rais Joe Biden, anaongoza kampeni ya chama chake cha Democratic mjini Maryland, ambako chama hicho kinatumai kuwa, kitashinda kiti cha Ugavana kutoka kwa chama cha Republican. Naye rais wa zamani Donald Trump, ataongoza kampeni za mwisho katika jimbo la Ohioa, kuwaombea wagombea wa chama cha Republican. AP
Matangazo ya kibiashara

Rais Joe Biden, anaongoza kampeni ya chama chake cha Democratic mjini Maryland, ambako chama hicho kinatumai kuwa, kitashinda kiti cha Ugavana kutoka kwa chama cha Republican. 

Naye rais wa zamani Donald Trump, ataongoza kampeni za mwisho katika jimbo la Ohioa, kuwaombea wagombea wa chama cha Republican. 

Mpaka sasa kura Milioni 41, zimeshapigwa kuelekea siku ya mwisho ya upigaji kura hapo kesho. 

Katika uchaguzi wa katikati ya muhula, hufanyika kila baada ya miaka miwili, ikiwa ni kipindi cha nusu cha uongozi wa rais aliye madarakani ili kubaini ni chama kipi kitadhibiti bunge la wawakilish na lile la Senate. 

Viti vyote vya wawakilishi 435 vinawaniwa lakini, thuluthi ya viti vya Maseneta vinawaniwa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.