Pata taarifa kuu

Mashambulizi mabaya nchini Canada: Mshukiwa wa pili afariki dunia baada ya kukamatwa

Myles Sanderson alifariki baada ya kukamatwa, vyombo vya habari vya Canada viliripoti Jumatano usiku. Pamoja na kaka yake, waliwaua watu kumi katika moja ya mashambulizi ya umwagaji damu zaidi nchini.

حمله با چاقو در کانادا
حمله با چاقو در کانادا AP - Michael Bell
Matangazo ya kibiashara

Mshukiwa wa hivi punde wa mashambulizi mabaya ya Jumapili ya nchini Canada alifariki baada ya kukamatwa na polisi siku ya Jumatano, vyombo kadhaa vya habari vilisema, likiwemo shirika la habari la Associated Press. Kulingana na vyanzo vya polisi ambavyo havikutajwa majina, magazeti kadhaa na vituo vya televisheni, ikiwa ni pamoja na redio na televisheni ya umma ya Canada CBC, vilitangaza kuwa mtu huyo mwenye umri wa miaka 32 amefariki, bila kutoa maelezo ya kina kuhusu mazingira ya kifo chake.

Jumatano jioni, polisi ilitangaza kukamatwa kwake kwenye mitandao ya kijamii: "Myles Sanderson alipatikana na kuwekwa chini ya ulinzi karibu na Rosthern, Saskatchewan, saa tisa na nusu."

"Hakuna hatari tena kwa usalama wa umma inayohusishwa na uchunguzi huu", polisi iliongeza, ikichukua fursa hiyo kuwashukuru wakaazi ambao walitoa "taarifa muhimu".

Mshukiwa huyo ambaye bado alikuwa na kisu alionekana baada ya kuiba gari katika eneo la takriban kilomita 100 kutoka eneo la uhalifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.