Pata taarifa kuu
USALAMA-HAKI

Mashambulizi Canada: Mmoja wa washukiwa apatikana amekufa, mwengine hajulikani aliko

Mmoja wa ndugu wawili wanaosakwa baada ya shambulio la Jumapili nchini Canada amepatikana amekufa, polisi imesema, wakati ikiendelea kumsaka mshukiwa wa pili wa mauaji haya, moja ya mauaji mabaya zaidi katika miaka ya hivi karibuni nchini humo na ambayo sababu zake bado hazijafahamika.

Ndugu wawili, Myles Sanderson na  Damien Sanderson, waliohusika katika shambulio la Jumapili nchini Canada.
Ndugu wawili, Myles Sanderson na Damien Sanderson, waliohusika katika shambulio la Jumapili nchini Canada. © 路透社图片
Matangazo ya kibiashara

Mmoja wa washukiwa wawili wa mashambulizi nchini Canada amefariki na mwili wake kupatikana Jumatatu (Septemba 5) katika mojawapo ya maeneo ambayo mauaji yalifanyika, polisi imesema.

Jumatatu joni, polisi ilitangaza kwamba wameupata mwili wa Damien Sanderson, ukiwa na majeraha kadhaa ya kisu, karibu na nyumba moja ambayo mashambulizi yalifanyika. "Hatuwezi kusema kwa uhakika jinsi Damian alikufa, lakini anaweza kuwa aliuawa na kaka yake," polisi imeongeza.

Myles Sanderson, ambaye pia inawezekana kuwa amejeruhiwa kwa mujibu wa polisi, bado anatafutwa. Alikuwa anajulikana kuwa alitumikia kifungo cha karibu miaka mitano kwa mashambulizi, wizi na vurugu. Baada ya kuachiliwa kwa dhamana, alipotea, hakurudi kuonekana tena na alikuwa akisakwa tangu mwezi Mei.

Mamia ya polisi bado wanamtafuta mshukiwa wa pili katika mfululizo wa mashambulizi ya visu, ambayo yalisababisha vifo vya watu kumi siku moja kabla katika miji miwili iliyojitenga katikati mwa nchi. Watu kumi na wanane pia walijeruhiwa, baadhi yao vibaya, katika kile kinachojumuisha moja ya mashambulizi ya umwagaji damu zaidi katika historia ya nchi. Kulingana na polisi, kuna matukio 13 ya uhalifu.

Mauaji hayo yalilenga jamii ya Wenyeji huko James Smith Cree Nation na mji wa karibu wa Weldon, Saskatchewan, mkoa mkubwa wa mashambani wenye wakazi wachache katikati mwa magharibi mwa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.