Pata taarifa kuu

Anga: Jaribio jipya la kuruka hadi mwezini kwa misheni ya NASA ya Artemis I

Miaka hamsini baada ya misheni ya Apollo na hatua za kwanza za Binadamu kutua mwezini, Shirika la Anga za Mbali la Marekani na Shirika la Anga la Ulaya zinazindua mpango wa Artemis.

Roketi ya NASA ya Space Launch System (SLS) ikiwa na chombo cha anga ya juu cha Orion, Jumanne, Agosti 30, 2022, katika Kituo cha Anga cha NASA cha Kennedy huko Cape Canaveral, Florida.
Roketi ya NASA ya Space Launch System (SLS) ikiwa na chombo cha anga ya juu cha Orion, Jumanne, Agosti 30, 2022, katika Kituo cha Anga cha NASA cha Kennedy huko Cape Canaveral, Florida. © AP - Joel Kowsky
Matangazo ya kibiashara

Misheni hii itaanzisha uwepo wa kudumu wa binadamu kwenye satelaiti, na ujenzi wa kituo cha anga katika obiti. Baada ya jaribio lililoshindwa siku tano zilizopita, misheni ya Artemis inapaswa kuanza Jumamosi hii, Septemba 3, pamoja na dirisha la kurusha la saa mbili, kuanzia saa nane na dakika kumi na saba mchana saa za huko, sawa na saa kumi na dakika kumi na saba alaasiri saa za ulimwengu.

Jaribio la kwanza lilikuwa Agosti 29. NASA ilikatizwa kurushwa kwa roketi ya Orion, ambayo ilikuwa iruke kutoka Cape Canaveral, Florida. Sababu, matatizo ya baridi kwenye moja ya injini.

Kasoro hiyo imerekebishwa, lakini hiyo haimaanishi kuwa uzinduzi huo utafanyika Jumamosi hii, Septemba 3. Ni utabiri wa hali ya hewa ambao unatia shaka.

Kuna uwezekano wa 60% wa mvua kunyesha na radi nyingi. Mwezi unaweza kusubiri kwa muda mrefu zaidi. Tarehe 5 Septemba imetajwa na mashirika ya anga ikiwa roketi hiyo haitaondoka Jumamosi hii.

Wataalamu wamezoea hatari zinazotangulia kuruka kwa roketi, na wanasalia kuwa na matumaini kwani vigingi vya misheni ya Artemis I ni vikubwa.

Safari hii ya ndege isiyo na rubani ya siku 42 ni ya kusukuma roketi yenye nguvu zaidi duniani kuzunguka satelaiti ili kuthibitisha kuwa chombo hiki kiko salama kwa wanaanga wa siku zijazo.

Kurudi halisi kwa binadamu, wanaume na hata wanawake, kutua mwezini kumepangwa mwaka 2025 au mapema zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.