Pata taarifa kuu

Hali mbaya ya hewa Brazil: Idadi ya vifo yaongezeka na kufikia zaidi ya watu 100

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na mvua kubwa iliyonyesha katika mji wa Petropolis nchini Brazili, ulioko katika eneo la milimani katika jimbo la Rio de Janeiro, imeongezeka siku ya Alhamisi hadi 104, kulingana na idara ya huduma za dharura.

Maafisa wa idara ya Zima moto na timu za ndani za ulinzi wa raia wanaendelea kufanya kazi kutafuta watu walio hai.
Maafisa wa idara ya Zima moto na timu za ndani za ulinzi wa raia wanaendelea kufanya kazi kutafuta watu walio hai. CARL DE SOUZA AFP
Matangazo ya kibiashara

Mvua hizi, ambazo kwa Jumanne pekee zilizidi wastani wa mwezi wa Februari, zilisababisha maporomoko ya ardhi yaliyosomba nyumba kadhaa.

Kwa upande wa Gavana wa Rio de Janeiro, Claudio Castro, amesema uharibifu unaosababishwa na hali mbaya ya hewa ni sawa "na hali ya vita".

Maafisa wa idara ya Zima moto na timu za ndani za ulinzi wa raia wanaendelea kufanya kazi kutafuta watu walio hai.

Rais wa Brazil Jair Bolsonaro ameahidi kuzuru maeneo yaliyoathiriwa siku ya Ijumaa baada ya kurejea kutoka nchini Urusi na Hungary kwa ziara ya kiserikali.

Tangu mwezi Desemba, mvua kubwa imesababisha mafuriko na maporomoko mabaya ya ardhi kaskazini mashariki na kusini mwa Brazili. Mvua hizi kubwa zinatishia kuchelewesha mavuno katika eneo la kati magharibi mwa nchi.

Maafisa wa idara ya Zima moto na timu za ndani za ulinzi wa raia wanaendelea kufanya kazi kutafuta watu walio hai.
Maafisa wa idara ya Zima moto na timu za ndani za ulinzi wa raia wanaendelea kufanya kazi kutafuta watu walio hai. © AP/Silvia Izquierdo
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.