Pata taarifa kuu
GUATEMALA-JAMII

Serikali na watu wa asili wafikia makubaliano baada ya mauaji magharibi mwa Guatemala

Magharibi mwa Guatemala, vizuizi vya barabarani kwenye barabara kuu ya Pan-American viliondolewa Jumanne, Desemba 21, baada ya makubaliano kati ya watu wa jamii ya asili na serikali.

Watu 13, wakiwemo watoto watatu, waliuawa wikendi iliyopita walipokuwa wakienda kuvuna mahindi katika eneo linalozozaniwa na jamii mbili za Maya.
Watu 13, wakiwemo watoto watatu, waliuawa wikendi iliyopita walipokuwa wakienda kuvuna mahindi katika eneo linalozozaniwa na jamii mbili za Maya. Johan ORDONEZ AFP
Matangazo ya kibiashara

Mamia ya watu wa kutoka jamii hiyo  walikuwa wamefunga barabara kwa siku mbili kudai hatua kadhaa zichukuliwe baada ya mauaji hayo mwishoni mwa juma lililopita: watu kumi na watatu, wakiwemo watoto watatu, waliuawa walipokuwa wakitoka kuvuna mahindi katika eneo linaloozozaniwa na jamii mbili za Maya.

Watu wa Nahuala na Santa Catarina Ixtahuacan wamekuwa wakiwindana kwa zaidi ya miaka 100. Jamii hizi mbili za Maya zinapigania upatikanaji wa ardhi, misitu na vyanzo vya maji, katika eneo hili lililo kilomita 170 magharibi mwa mji mkuu. Mwaka jana, baada ya wimbi jingine la vurugu, serikali  iliwakamata makumi ya watu, silaha na risasi, bila kukomesha uhasama huo.

Mamia ya watu wa kiasili ambao walifunga barabara kuu ya Pan-American kwa siku mbili wanaitaka serikalikushughulikia tatizo la msingi: kuweka wazi mipaka ya maeneo ya vijiji hivyo viwili.

Mazungumzo mapya

Jumanne, Desemba 21, mameya wa Nahuala na Santa Catarina Ixtahuacan, gavana wa eneo hilo pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani walikubaliana wakati wa mkutano wa faragha katika Jiji la Guatemala juu ya ufunguzi wa mazungumzo mapya ya kujaribu kutatua mzozo huu wa zamani wa ardhi, inayosababisha maafa makubwa katika eneo hilo. Mazungumzo hayo yamepangwa kuanza katikati ya mwezi wa Januari.

Kufikia sasa, majaribio mengine ya majadiliano yameshindwa, hasa yale yaliyoongozwa na makamu wa rais wa Guatemala. Kwa sasa, Baraza la Wwakilishi limeidhinisha sheria ya rais ambayo inaweka vijiji hivi viwili chini ya sheria ya kijeshi kwa siku 30.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.