Pata taarifa kuu
GUATEMALA-USALAMA

Sita wafariki dunia baada ya ghasia katika jela la magharibi mwa Guatemala

Watu sita wameuawa katika gereza moja magharibi mwa Guatemala baada ya ghasia kuzuka katika kituo hicho Jumatano, viongozi wamesema katika taarifa.

Maafisa wa polisi ya kupambana na ghasia wanaingia gerezani baada ya ghasia kuzuka katika jela moja, katika manispaa ya Cantel, huko Quetzaltenango, Guatemala Mei 19, 2021.
Maafisa wa polisi ya kupambana na ghasia wanaingia gerezani baada ya ghasia kuzuka katika jela moja, katika manispaa ya Cantel, huko Quetzaltenango, Guatemala Mei 19, 2021. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Waathiriwa walipatikana wamekatwa vichwa katika gereza lililojaa wafungwa wengi katika mji wa Cantel, katika jimbo la Quetzaltenango, kulingana na taarifa ya polisi.

Chanzo cha polisi, ambacho hakikutaka jina lake litajwe, kimesema mauaji hayo yalikuwa sehemu ya makabiliano kati makundi mawili hasimu yanayofanya biashara haramu ya dawa za kulevya.

Polisi inahakikisha kuwa imerejesha hali ya utulivu katika jela hilo. Jemla hili lina wafungwa kutoka makundi mawili hasimu Mara Salvatrucha na Barrio 18, pamoja na wafanyabiashara ya dawa za kulevya, shirika la habari la AFP limeripoti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.