Pata taarifa kuu
GUATEMALA-SIASA

Guatemala: Maelfu ya waandamanaji wamtaka rais ajiuzulu

Maelfu ya raia nchini Guatemala wameendelea kumiminika mitaani kutaka rais Alejandro Giammattei ajiuzulu baada ya kufutwa kazi kwa mwendesha mashtaka anaye pambana dhidi ya ufisadi.

Raiw wa Guatemala Alejandro Giammattei.
Raiw wa Guatemala Alejandro Giammattei. Orlando ESTRADA AFP
Matangazo ya kibiashara

Wiki iliyopita, Mwanasheria Mkuu Maria Porras alimfukuza kazi Juan Francisco Sandoval kama mkuu wa ofisi ya mwendesha mashtaka maalum dhidi ya ukatili, hatua iliyolaaniwa na Washington.

Juan Francisco Sandoval, ambaye aliondoka Guatemala, alisema alizuiwa kuchunguza kesi za ufisadi zinazamkabili rais wa Guatemala.

Katika Jiji la Guatemala, maelfu ya raia waliandamana Alhamisi wiki hii mbele ya ikulu ya rais na ofisi ya wakili mkuu, wakishikilia mabango yaliyoandikwa "Giammattei, jiuzulu!"

Waandamanaji hao walichoma moto matairi na kuwarushi rangi maafisa wa polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.