Makao makuu ya Bunge yachomwa moto Guatemala
Maelfu ya watu wameandamana na kukusanyika kwa amani katika eneo kuu la Jiji la Guatemala (mji mkuu) Jumamosi, Novemba 21 wakipinga dhidi ya kupunguzwa kwa bajeti, hatua iliyochukuliwa na serikali.
Imechapishwa:
Kando na maandamano hayo, waandamanaji wengine wenye hasira walichoma moto makao makuu ya Bunge la nchi hiyo. Waandamanaji hao walikuwa wamebebelea bendera za nchi hiyo na mabango yaliyoandikwa "Giammattei, ajiuzulu".
Waandamanaji hao wametoa wito kwa rais Alejandro Giammattei kupinga bajeti hiyo iliyopitishwa Jumatano ya wiki hii.
"Bunge limetenga pesa zaidi kwa manufaa yake ikilinganishwa na pesa zilizotengwa kwa maskini," amesema Diego Herrera, mwanafunzi wa miaka 25, ambaye ni mmoja wa waandamanaji hao wenye hasira.
Hali ya sintofahamu inaendelea kuripotiwa katika miji mbalimbali ya Guatemala.