Pata taarifa kuu
BRAZIL-HAKI

COVID-Brazil: Ripoti inayomshutumu rais Bolsonaro yaidhinishwa

Ripoti ya Kamati ya Seneti nchini Brazil kuhusu Covid-19 iliyokuwa inamuelemea rais wa nchi hio Jair Bolsonaro imeidhinishwa kwa kura saba dhidi ya nne.

Katika ripoti hii ya Seneti inayokaribia kurasa 1,200, Rais Jair Bolsonaro (picha yetu), ambaye amekuwa akikana uzito wa virusi hivyo, anashutumiwa kwa "uhalifu dhidi ya binadamu."
Katika ripoti hii ya Seneti inayokaribia kurasa 1,200, Rais Jair Bolsonaro (picha yetu), ambaye amekuwa akikana uzito wa virusi hivyo, anashutumiwa kwa "uhalifu dhidi ya binadamu." EVARISTO SA AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Maseneta kumi na mmoja wa tume ya bunge ya uchunguzi walinyamaza kwa dakika moja kuwakumbuka zaidi ya watu 600,000 waliofariki kutokana na Covid-19, baada ya kikao kilichoidhinisha Jumanne, Oktoba 26 ripoti ya wajibu wa serikali katika mgogoro wa afya.

Baada ya miezi sita ya uchunguzi na vikao kadhaa, tume ilishutumu serikali kwa "kuwaweka hatarini kimakusudi" Wabrazil kwa "maambukizi makubwa" ya virusi vya Corona.

"Uhalifu dhidi ya binadamu"

Katika ripoti hiyo ya karibu kurasa 1,200, rais Jair Bolsonaro, ambaye amekuwa akikana uzito wa virusi hivyo, anashtakiwa kwa "uhalifu dhidi ya binadamu" na anaweza kufikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.

Anashutumiwa pia kwa "kosa la janga linalosababisha kifo", "uchochezi wa uhalifu", kwa kutetea matumizi ya chloroquine katika matibabu ya wagonjwa wa Covid. Jumla anakabiliwa na mashitaka tisa.

Mashitaka yasiyowezekana

Ripoti hii, ambayo inawatuhumu watu 80, wakiwemo mawaziri kadhaa, mawaziri wa zamani, makampuni na wahudumu wakubwa wa afya wa Bolsonaro, viongozi wote waliochaguliwa, itakabidhiwa kwa upande wa mashtaka Jumatano, na ni Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri, Augusto Aras, mshirika wa rais wa Brazil, ambaye ataamua iwapo atawafungulia mashtaka au la.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.