Brazil yaendelea kukumbwa na maandamano, COVID-19 yaendelea kushika kasi
Brazil inaendelea kukumbwa na maandamano wakati idadi ya visa vya maabukizi na vifo inaendelea kuonezeka kila kukicha.
Imechapishwa:
Maelfu ya watu waliandamana Jumatano jioni, wakati Rais Jair Bolsonaro akihutubia taifa, siku chache tu baada ya waandamanaji kuingia barabarani nchini humo kupinga jinsi anavyoshughulikia janga la COVID-19, ambalo hadi sasa limeuwa karibu watu nusu milioni nchini humo.
Serikali ya kiongozi wa mrengo wa kulia imeendelea kukabiliwa na hali ngumu kutokana na kushindwa kushughulikia janga la COVID-19.
Kuendelea kwa idadi kubwa ya vifo na visa vya kila siku vya maambukizi ya COVID-19 kumedhoofisha umaarufu wa Rais Jair Bolsonaro.
Siku ya Jumatano pekee, karibu Wabrazil 100,000 waliam janga hiloyo, kulingana na takwimu za serikali.