Pata taarifa kuu
BRAZILI

COVID: Makumi ya maelfu ya Wabrazil wamtaka Bolsonaro kujiuzulu

Makumi ya maelfu ya Wabrazil walimiminika mitaani Jumamosi, wakitaka rais Jair Bolsonaro kujiuzulu kwa jinsi anavyoshughulikia mgogoro wa kiafya wakati idadi ya vifo kutokana na janga hilo imezidi nusu milioni, kulingana na shirika la habari la AFP.

Mmoja wa waandamanaji akivaa fulana na kinyago wakati wa maandamano wakishtumu usimamizi mbaya katika kushughulikia janga la COVID, Januari 23, 2021.
Mmoja wa waandamanaji akivaa fulana na kinyago wakati wa maandamano wakishtumu usimamizi mbaya katika kushughulikia janga la COVID, Januari 23, 2021. AFP - SERGIO LIMA
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji waliandamana kwa siku ya Jumamosi kwa wiki ya nne mfululizo wakiitikia wito wa vyama vya mrengo wa kushoto na vyama vya wafanyakazi, hasa dhidi ya rais wa mrengo wa kulia, ambaye anachunguzwa kwa madai ya kufumbia macho ubadhirifu wa fedha za umma katika ununuzi wa chanjo.

Huko Rio, maelfu ya watu waliovaa nguo nyekundu na barakoa waliandamana wakitoa maneno kama vile "ondoka mhalifu mbaya anayenuka ufusadi".

Waandaaji walikuwa wameitisha maandamano kote nchini "kutetea demokrasia, maisha ya Wabrazil na kumtoa Bolsonaro".

Huko Rio kama mahali pengine, waandamanaji walishutumu mwanzo wa kampeni ya chanjo hnchini Brazil, ukosefu mkubwa wa ajira, na kutaka msaada zaidi kwa watu maskini wanaokabiliwa na janga hilo.

"Ni muhimu sana kwamba mtu yeyote ambaye anahisi kukerwa au kuonewa na serikali hii ajitokeze barabarani kwa sababu tunapaswa kupigania kurudi kwa demokrasia," Laise de Oliveira, mfanyakazi wa huduma za kijamii mwenye umri wa miaka 65 ameliambia shirika la habarila AFP.

Vyombo vya habari vya Brazil vimeripoti kuwa maandamano ya jana alasiri yalifanyika katika majimbo 20 kati ya 26 ya Brazil.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.