Coronavirus: Vifo vipya 721 vyaripotiwa Brazil katika muda wa saa 24
Brazil imerekodi vifo vipya 721 vinavyohusiana na COVID-19 na kesi mpya 34,027 zilizothibitishwa jana Jumapili, kulingana na takwimu zilizotolewa na Wizara ya Afya.
Imechapishwa:
Wizara hiyo inabaini kwamba visa vimepungua kidogo baada ya siku tano mfululizo zilizogubikwa na vifo visivyopungua 1,300 na visa 60,000 vya maambukizi ya kila siku.
Brazil imerekodi jumala ya vifo 254,942 vinavyohusishwa na janga hilo tangu ugonjwa huo kuzuka nchini humo.
Hayo yanajiri wakati Marekani Jumamosi Februari 27 iliidhinisha chanjo ya kampuni ya Jonhson & Johnson kwa matumizi ya dharura, na kuipatia nchi hiyo chanjo ya tatu ya kukabiliana na janga la virusi vya Corona ambavyo vimeua watu 500,000 nchini humo.
Mamlaka ya chakula na dawa, FDA, imethibitisha kuwa chanjo ya Johnson&Johnson itatolewa kwa watu wenye umri wa kuanzia miaka 18 na zaidi.
Kuidhinishwa kwake kunaongeza nguvu kwenye kampeni ya taifa ya utoaji chanjo nchini Marekani ambayo ilisuasua kwa wiki kadhaa.
Karibu raia milioni 47.2 wa Marekani tayari wamepatiwa dozi ya kwanza ya chanjo ya corona, kulingana na taasisi ya kupambana na magonjwa nchini humo.