Pata taarifa kuu
BRAZIL-USALAMA-MAANDAMANO

Brazil: Watu wapandwa na hasira baada ya kifo cha mtu mweusi aliyepigwa na walinzi

Maelfu ya watu wenye hasira wameendelea kuandamana katika mitaa ya miji mbalimbali nchini Brazil bada ya kifo cha mtu mweusi, aliyepigwa na walinzi wazungu katika duka kubwa la kampuni ya Carrefour huko Porto Alegre, Kusini mwa nchi.

Baadhi ya waandamanaji walirusha mawe na kuvunja vio vya duka hilo kabla ya kulivamia, na kuharibu au kuchoma moto bidhaa mbalimbali, madirisha na vifaa vingine, kulingana na mpiga picha wa shirika la habari la AFP.
Baadhi ya waandamanaji walirusha mawe na kuvunja vio vya duka hilo kabla ya kulivamia, na kuharibu au kuchoma moto bidhaa mbalimbali, madirisha na vifaa vingine, kulingana na mpiga picha wa shirika la habari la AFP. AFP
Matangazo ya kibiashara

Jana Ijumaa maelfu ya waandamanaji waliandamana katikati ya jiji la Sao Paulo hadi duka la kampuni ya Carrefour katika kitongoji cha Jardim Paulista.

Baadhi yao walirusha mawe na kuvunja vio vya duka hilo kabla ya kulivamia, na kuharibu au kuchoma moto bidhaa mbalimbali, madirisha na vifaa vingine, kulingana na mpiga picha wa shirika la habari la AFP.

"Mikono ya kampuni ya Carrefour imechafuliwa na damu nyeusi", maneno ambayo yaliandikwa kwenye moja ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na waandamanaji.

Katika mji wa Porto Alegre, ambapo mtu huyo mweusi alifariki dunia kutokana na kipigo cha maafisa wa usalama, polisi ilisambaratisha maandamano kwa mabomu ya machozi, kulingana na kituo cha televisheni ya umma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.