Pata taarifa kuu
CANADA-CHINA-USHIRIKIANO

Ottawa yaitaka Beijing kuwaachilia huru raia wake wawili

Waziri wa Mambo ya nje wa Canada François-Philippe Champagne amekutana huko Roma na mwenzake wa China Wang Yi na ameitaka China iwachilie huru raia wa Canada wanaozuiliwa nchini humo, serikali ya Canada imesema.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada François-Philippe Champagne na mwenzake wa China Wang Yi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada François-Philippe Champagne na mwenzake wa China Wang Yi REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo wa nje wa Canada pia ameonyesha msimamo wa Ottawa kupinga udhalimu unaofanywa na Beijing kwa wakazi wa Hong Kong, amesema afisa mmoja wa Canada ambaye hakutaka jina lake litajwe kutokana na hali ya usalama.

François-Philippe Champagne amezungumza na Wang Yi katika hoteli moja ya mji mkuu wa Italia kwa dakika 90. Wawili hao walikutana hapo awali mwezi Novemba.

Uhusiano baina ya Canada na China umezorota tangu kukamatwa kwa mkurugenzi wa masuala ya fedha wa kampuni ya simu ya Huawei kutoka China, Meng Wanzhou, huko Vancouver mwezi Desemba 2018.

Washington inataka Meng Wanzhou asafirishwe nchini Marekani.

Muda mfupi baadae, vmamlaka nchini China ililwakamata raia wa Canada Michael Spavor na Michael Kovrig kwa madai ya kuiba siri za serikali.

"Waziri Champagne amesisitiza kwamba kesi ya Michael Kovrig na Michael Spavor imebaki kuwa kipaumbele cha hali ya juu (...) na kwamba Canada itaendelea kuitaka China kuwaachilia huru mara moja," imebaini taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Canada.

Wang amemwambia Champagne kwamba uamuzi wa Canada kuwakamata raia wa China bila kuwa na hatia yoyote umesababisha 'hali ya sintofahamu' katika uhusiano wa nchi hizo mbili, Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema.

Katika taarifa yake, wizara hiyo imeongeza kuwa Wang ameitaka serikali ya Canada kuchukua hatua haraka iwezekanavyo ili kuondoa vizuizi kwa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Canada.

Wawili hao pia "wamejadili umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika kupambana dhidi ya ugonjwa wa COVID-19, pamoja na utaftaji wa chanjo," imesema Wizara ya Mambo ya Nje ya Canada.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.